Rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva
***
Viongozi wa
mashtaka nchini Brazil wanasema kuwa watamfungulia mashtaka ya kujipatia
fedha kwa njia haramu aliyekuwa rais wa taifa hilo, Luiz Inacio Lula da
Silva.
Wanasema kuwa bwana Lula pamoja na mkewe walishindwa
kutangaza umiliki wao wa nyumba moja ya kifahari kwenye ufukwe wa bahari
katika eneo la Guaruja.
Rais huyo wa zamani ambaye ni mashuhuri kwa sasa nchini Brazil amekanusha madai hayo akisema kuwa yamechochewa kisiasa.
Nyumba
hiyo inamilikiwa na kampuni moja ya ujenzi ambayo imehusishwa na sakata
moja kubwa katika kampuni ya mafuta ya serikali ya Petrobras. CHANZO: BBCSWAHILI.COM |
No comments:
Post a Comment