DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, March 10, 2016

AMANI WA KENYA AJA NA "BONBON" AKIMSHIRIKISHA WASHINGTON

Yupo kwenye orodha ya wanamuziki wakongwe kwenye muziki wa kizazi kipya nchini Kenya…. wengi wanazikumbuka hits zake kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 2000 na bado mpaka sasa hajatangaza kuacha kuingia studio… katuletea hii single mpya ‘bonbon‘ yuko na Washington.

RAIS WA VIETINAM AHUTUBIA MKUTANO WA BAIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA VIETINAM JANA

Rais wa Vietinam, Trung Tan Sang akizungumza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kabla ya kuanza kwa mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016.
Baadhi ya washiriki wa  mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam uliofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016. 
Rais wa Vietinam, Trung Tan Sang akiteta  na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika  mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Vietinam, Trung Tan Sang kuhutubia  mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016.
Rais wa Vietinam, Trung Tan Sang akihutubia mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016.
Rais wa Vietinam, Trung Tan Sang akimpongeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alizungumza na kumkaribisha Rais huyo kuhutubia   mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016.
Rais wa VietinamTrung Tan Sang (kuliakwa Waziri Mkuu) na Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja badhi ya viongozi na wafanyabiashara wa Tanzania na Vietinam  baada ya mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016. (Picha zote na ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MBARAWA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA FLOW METER ZA KUPIMIA MAFUTA PAMOJA NA KIVUKO CHA MV KIGAMBONI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa Meneja ujenzi wa kampuni ya BQ Bw. Neven Slavujevic  inayojenga mtambo wa kupima mafuta bandarini (flow meter ) kwenye kituo cha kupakulia mafuta kilichopo Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akipanda juu ya mtambo wa kupima mafuta bandarini (flow meter) kwa ajili ya kuukagua kwenye kituo cha kupakulia mafuta kilichopo Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es salaam.
Meneja ujenzi wa kampuni ya BQ Bw. Neven Slavujevic  inayojenga mtambo wa kupima mafuta bandarini (flow meter )akifafafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa alipokagua mtambo huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa wajenzi wa Flow Meter ya Mji mwema.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza mmoja wa abiria wanaotumia kivuko cha Magogoni kabla  ya kukikagua.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza mtaalam wa kivuko eneo la Magogoni jijini Dar es salaam wakati alipokagua kivuko cha MV Kigamboni na MV Magogoni kuona utendaji wake.

KUPATWA KWA JUA KWATOKEA NCHINI INDONESIA

Watu wamelitaja tukio hilo la miujiza. Raia Indonesia wameshuhudia jua likizibwa kikamilifu na mwezi.
Indonesia ndio nchi pekee iliyoshuhudia tukio hilo kote duniani.
Mamia ya watu walimiminika kushuhudia jua likinaswa na mwezi.
*** 
Hoteli zilizopo katika maeneo mazuri ya kushuhudiwa jua likinaswa zilijaa miezi kadhaa iliopita na katika baadhi ya maeneo ilibidi maafisa watafute nafasi za ziada kwa watalii waliokuwa kwenye maboti.
Katika kisiwa cha Belitung mamia ya wageni na watalii wa nchni walikusanyika katika fukwe za bahari kabla ya alfajiri. Wakati jua lilipoanza kunaswa na mwezi walishangilia na baadaye kunyamaza kimya kwa mshangao.
Wengi wamelielezea tukio hilo kama 'tukio la miujiza'. Kwa wengi Indonesia, tukio hilo linashirikishwa sana na dini na watu huomba, sherehe za kitamaduni na ngoma zimeandaliwa katika sehemu kubwa la eneo hilo.
Wanasayansi pia wamkuwepo hususan katika eneo la Maba katika visiwa vya Maluku ambako tukio hilo limeshuhudiwa kwa dakika tatu, ambao ni muda mrefu kuwahi kushuhudiwa jua likinaswa na mwezi. CHANZO: BBCSWAHILI.COM

MTAALAM WA KEMIKALI WA KUNDI LA IS AKAMATWA

Wapiganaji wa Islamic State 
*** 
Mtaalamu wa masuala ya silaha za kemikali katika wapiganaji wa Islamic State nchini Iraq amekamatwa na vikosi maalum vya Marekani na sasa anahojiwa.
Mtu huyo alikuwa mtaalamu wa masuala ya silaha za kibaiolojia wa aliyekuwa rais wa Iraq Sadam Hussein ,aliyepinduliwa na uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka 2003, duru za Iraq na zile za Marekani zimeambia vyombo vya habari vya Marekani.
Akijulikana kama Sleiman Daoud Al_fari,aliripotiwa kukamatwa mwezi uliopita.
Hatahivyo, msemaji wake amesema kuwa vikosi maalum vya Marekani vimeanza oparesheni zake nchini Iraq, ikiwa ni mwanzo wa vita vikali dhidi ya Islamic State.
Mtu huyo amewaambia wanaomuhoji vile kundi la Islamic State lilivyotumia gesi ya sumu katika makombora yake, duru za Marekani zimeliambia gazeti la "The New York Times". CHANZO: bbcswahili.com

LULA DA SILVA KUFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA HARAMU

Rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva 
*** 
Viongozi wa mashtaka nchini Brazil wanasema kuwa watamfungulia mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia haramu aliyekuwa rais wa taifa hilo, Luiz Inacio Lula da Silva.
Wanasema kuwa bwana Lula pamoja na mkewe walishindwa kutangaza umiliki wao wa nyumba moja ya kifahari kwenye ufukwe wa bahari katika eneo la Guaruja.
Rais huyo wa zamani ambaye ni mashuhuri kwa sasa nchini Brazil amekanusha madai hayo akisema kuwa yamechochewa kisiasa.
Nyumba hiyo inamilikiwa na kampuni moja ya ujenzi ambayo imehusishwa na sakata moja kubwa katika kampuni ya mafuta ya serikali ya Petrobras. CHANZO: BBCSWAHILI.COM

JIFUNZE KISWAHILI FASAHA NA SANIFU CHA MANENO HAYA YA KIINGEREZA: KITCHEN PARTY, SMARTPHONE, EXPIRE, LIVE NA SEND-OFF PARTY

Inawezekana Kiswahili ikawa ni lugha yako ya kwanza lakini bado kuna vitu vingi tu huvijui au huwa hauvitamki kwa Kiswahili ndio maana leo nimeamua kukutanisha na maana ya maneno machache ambayo tumezoea kuyatamka kwa kiingereza japo tunayaongea kwenye sentensi zenye kiswahili.
Neno LIVE mfano pale unaposema CloudsTV inaonyesha LIVE… kwa Kiswahili LIVE ni PAPO, sasa hivi pia tunazo simu za kisasa ambazo tunaziita Smartphones ila kwa Kiswahili jina lake ni SIKANU……. pia kwenye ile sherehe maarufu kwa jina la Send-off kwa kiswahili ni ‘sherehe ya Mwago‘ kwa sababu Binti ndio anaagwa.
Kuna kitu kinaitwa Kitchen Party ambapo kiswahili chake ni ‘JIKO MTAWAZO‘ yaani mtu anatawazwa kuhusu mambo ya jiko na mambo ya maisha ndio maana mtu akioa Waswahili wanasema umepata Jiko.
Neno jingine la kufahamu kwa leo ni pale unapokuta kitu au bidhaa imekwisha muda wake wa matumizi mfano maziwa au mkate, neno maarufu tunalitumia ni ‘expire‘ ila kwa Kiswahili fasaha unaambiwa ni ‘IMECHOTORA'. CHANZO: millardayo.com

FC BARCELONA YATOA RAMANI YA UWANJA MPYA UNAOTARAJIWA KUJENGWA NA KUKAMILIKA IFIKAPO 2021

Klabu ya FC  Barcelona ya Hispania ambayo imezoeleka kutumia uwanja wake wa Nou Camp, Machi 9, 2016 imetoa picha za muonekano wa uwanja wao utakavyokuwa kwa miaka minne ijayo. FC Barcelona wametoa picha za ramani ya ujenzi wa uwanja huo ambao utajengwa kwa thamani ya Pound milioni 465.



Mabingwa hao wa Ulaya wamethibitisha kuwa mchora ramani na mbunifu wa Kijapan Nikken Sekkei ndio ameshimda tenda ya kufanya ukarabati wa uwanja huo hadi utakapokamilika 2021, ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 105000.

RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA MAALIM SEIF HOTELINI

Amekua akisema siku zote kwamba yeye ni Rais wa Watanzania wote bila kujali vyama wala dini ndio maana Machi 9, 2016 Dkt. John Magufuli alimtembelea na kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad kwenye hoteli ya Serena Dar es Salaam ambako anapata mapumziko baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Hindu Mandal alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

RAIS WA VIETNAM , TRUONG TAN SANG ALIVYOKARIBISHWA IKULU YA DAR ES SALAAM


Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe mama Mai Thi Hanh wakiwasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.

Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akipokea zawadi ya ua toka kwa mtoto mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 akiwa amefuatana na mmewe kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kushoto) akimkaribisha mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye koti la drafti) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli. CHANZO: mjengwablog.com

RAIS WA JAMHURI YA KISOSHALISTI YA VIETNUM TRUONG TAN SANG ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA CCM YALIYOPO OFISI NDOGO LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Machi 09, 2016. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya faragha ofisini kwake na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini.
 Waziri wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga akizungumza na Katibu wa NEC anayeshughulikia Uchumi na Fedha wa CCM, Zakiah Megji wakati wa mazungumzo ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na mgeni wake, Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana.
Katibu wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akiwa na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatibu wakati wa mazungumzo hayo ya Kikwete na Rais wa Vietnam. Kulia Ni Kaim Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Shaka Hamidu Shaka.
Viongozi na Maofisa wa CCM wakiwa kwenye mazungumzo hayo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.  Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga na kulia ni Dk. Asha-Rose Migiro.
Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo hayo.

MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA SHINYANGA

Hapa ni katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa Uboreshaji Mifumo ya Sekta za Umma unaojulikana kwa jina la Public Sector Systems Strenghening (PS3) unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Lengo la mradi huo ni kuimarisha mifumo ya ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora,rasilimali watu,fedha utoaji taarifa na tafiti tendaji katika halmashauri za wilaya na taifa kwa ujumla.
Mkutano wa uzinduzi huo utakaofanyika kwa siku mbili Machi 09,2016 hadi Machi 10,2016 umehudhuriwa na Kiongozi wa timu ya mradi,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga,wakuu wa wilaya,meya wa manispaa ya Shinyanga,wenyeviti wa halmashauri za wilaya,wataalam kutoka kutoka ofisi ya Waziri mkuu na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi,mashirika na taasisi za umma na binafsi-Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde yupo eneo la tukio ametusogezea picha 30 ,Tazama hapa chini

Kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe ambaye pia ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma Public Sector Systems Strenghening(PS3) utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitano na utafanya kazi na serikali kuu pamoja na halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.

Wakuu wa wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini,wa kwanza kushoto ni Vita Kawawa kutoka wilaya ya Kahama, akifuatiwa na Josephine Matiro kutoka wilaya ya Shinyanga na Hawa Ng’umbi kutoka wilaya ya Kishapu.
Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizindua mradi wa PS3 ambapo alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa 13 nchini ambayo itanufaika na mradi huo ambapo alidai umeanza kwa wakati muafaka kwani sasa serikali iliyopo madarakani inataka mabadiliko katika kuhakikisha kuwa serikali inahudumia wananchi ipasavyo.
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (kushoto) akifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.Rufunga alisema mradi huo utakuwa na tija kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga.

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUUNDA MAMLAKA KUU YA MAPATO YA TAIFA

Kaimu Kamishna wa TRA Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano wa kutoa taarifa juu ya ukusanyaji wa kodi kwa mwezi Februari, 2016.
Serikali ipo kwenye mpango wa kuunda Mamlaka ya Mapato Kuu ya Taifa nje ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo kwa sasa ili kuondokana na malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Alphayo Kidata alipokuwa akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kuweza kumudu kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na na Mamlaka hiyo.
“ Napenda kuwaambia umma wa watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya tano inawajali watu wake na ndio maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda Mamlaka moja ya utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko mengi ya wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika Halmashauri zetu”Alisema Kidata.
“Kamishna Kidata amesema kuwa katika dunia hii hakuna Serikali ambayo imechaguliwa na wananchi ikaamua tu kuwakandamiza wananchi wake katika jambo lolote lile hivyo basi kwa sasaserikali ipo katika mchakato wa kuunda Mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi wanazozifanya.
Kamishna huyo ameongeza kuwa Mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazokusanya kodi katika Halmashauri nchini watahakikisha wanalipatia ufumbuzi suala la kero ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata muafaka ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote iwe Serikali ama mwananchi wa kawaida.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi ila kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi ambazo zimekuwa kero na hazina tija. Hivyo Serikali imejipanga kuiongezea nguvu Mamlaka hiyo kwa kuipa uwezo wa kukusanya na mapato ambayo hayatokani na kodi toka katika wizara, mashirika,tasisi za serikalina Halmashauri zote nchini.



MAGAZETI ALHAMISI YA MACHI 10,2016