DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, March 10, 2016

RAIS WA JAMHURI YA KISOSHALISTI YA VIETNUM TRUONG TAN SANG ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA CCM YALIYOPO OFISI NDOGO LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Machi 09, 2016. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya faragha ofisini kwake na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini.
 Waziri wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga akizungumza na Katibu wa NEC anayeshughulikia Uchumi na Fedha wa CCM, Zakiah Megji wakati wa mazungumzo ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na mgeni wake, Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana.
Katibu wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akiwa na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatibu wakati wa mazungumzo hayo ya Kikwete na Rais wa Vietnam. Kulia Ni Kaim Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Shaka Hamidu Shaka.
Viongozi na Maofisa wa CCM wakiwa kwenye mazungumzo hayo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.  Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga na kulia ni Dk. Asha-Rose Migiro.
Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo hayo.

MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA SHINYANGA

Hapa ni katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa Uboreshaji Mifumo ya Sekta za Umma unaojulikana kwa jina la Public Sector Systems Strenghening (PS3) unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Lengo la mradi huo ni kuimarisha mifumo ya ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora,rasilimali watu,fedha utoaji taarifa na tafiti tendaji katika halmashauri za wilaya na taifa kwa ujumla.
Mkutano wa uzinduzi huo utakaofanyika kwa siku mbili Machi 09,2016 hadi Machi 10,2016 umehudhuriwa na Kiongozi wa timu ya mradi,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga,wakuu wa wilaya,meya wa manispaa ya Shinyanga,wenyeviti wa halmashauri za wilaya,wataalam kutoka kutoka ofisi ya Waziri mkuu na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi,mashirika na taasisi za umma na binafsi-Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde yupo eneo la tukio ametusogezea picha 30 ,Tazama hapa chini

Kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe ambaye pia ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma Public Sector Systems Strenghening(PS3) utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitano na utafanya kazi na serikali kuu pamoja na halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.

Wakuu wa wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini,wa kwanza kushoto ni Vita Kawawa kutoka wilaya ya Kahama, akifuatiwa na Josephine Matiro kutoka wilaya ya Shinyanga na Hawa Ng’umbi kutoka wilaya ya Kishapu.
Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizindua mradi wa PS3 ambapo alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa 13 nchini ambayo itanufaika na mradi huo ambapo alidai umeanza kwa wakati muafaka kwani sasa serikali iliyopo madarakani inataka mabadiliko katika kuhakikisha kuwa serikali inahudumia wananchi ipasavyo.
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (kushoto) akifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.Rufunga alisema mradi huo utakuwa na tija kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga.

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUUNDA MAMLAKA KUU YA MAPATO YA TAIFA

Kaimu Kamishna wa TRA Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano wa kutoa taarifa juu ya ukusanyaji wa kodi kwa mwezi Februari, 2016.
Serikali ipo kwenye mpango wa kuunda Mamlaka ya Mapato Kuu ya Taifa nje ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo kwa sasa ili kuondokana na malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Alphayo Kidata alipokuwa akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kuweza kumudu kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na na Mamlaka hiyo.
“ Napenda kuwaambia umma wa watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya tano inawajali watu wake na ndio maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda Mamlaka moja ya utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko mengi ya wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika Halmashauri zetu”Alisema Kidata.
“Kamishna Kidata amesema kuwa katika dunia hii hakuna Serikali ambayo imechaguliwa na wananchi ikaamua tu kuwakandamiza wananchi wake katika jambo lolote lile hivyo basi kwa sasaserikali ipo katika mchakato wa kuunda Mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi wanazozifanya.
Kamishna huyo ameongeza kuwa Mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazokusanya kodi katika Halmashauri nchini watahakikisha wanalipatia ufumbuzi suala la kero ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata muafaka ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote iwe Serikali ama mwananchi wa kawaida.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi ila kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi ambazo zimekuwa kero na hazina tija. Hivyo Serikali imejipanga kuiongezea nguvu Mamlaka hiyo kwa kuipa uwezo wa kukusanya na mapato ambayo hayatokani na kodi toka katika wizara, mashirika,tasisi za serikalina Halmashauri zote nchini.



MAGAZETI ALHAMISI YA MACHI 10,2016























PSG YAIRARUA CHELSEA 2-1 LIGI YA MABINGWA ULAYA




Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, iliyochezwa usiku wa Machi 09, 2016 kwenye viwanja viwili tofauti,  ikiwemo uwanja wa Stamford Bridge uliyopo jijini London na Petrovsky uliopo nchini Urusi.
Jiji la London, wenyeji Chelsea wamelazimika kuchezea kichapo cha pili mfululizo toka kwa PSG kutoka jijini Paris nchini Ufaransa kwa kufungwa bao 2-1, ambapo ushindi huo ni kama ule walioupata timu hiyo ya PSG katika mchezo wao wa awali na kwa maana hiyo, PSG wameweza kujipatia pointi 6 muhimu na magoli 4, huku Chelsea wao wakiambulia mabao yao 2.
Kwa hatua hiyo, PSG  anaingia hatua ya robo fainali katika michuano hiyo mikubwa kabisa barani Ulaya. PSG ilikuwa inahitaji ushindi wa aina yoyote ili kuweza kusonga mbele au sare, hivyo kwa ushindi huo imefuzu hatua ya robo fainali.
Mchezo mwingine umechezwa nchini Urusi , wenyeji Zenit wameweza kulala kwa bao 2-1 dhidi ya Benfica ya nchini Ureno.
Katika mchezo wa awali Benfica walikuwa nyumbani na walifanikiwa kushinda bao 1-0, kwa hatua hiyo Benfica wamefanikiwa kuingia hatua ya robo  ya michuano hiyo kwa jumla ya poiti 6 huku ikijipatia mabao 3, dhidi ya moja la wapinzani wao hao.

Mchezaji wa PSG, Ibrahimovic akipachika bao  wavuni dhidi ya Chelsea usiku wa kuamkia leo na kufanya matokeo 2-1.

Mchezaji wa PSG, Ibrahimovic akishangilia bao lake aliloifungia PSG  dhidi ya Chelsea usiku huu na kufanya matokeo 2-1.Taarifa hizi ni kwa msaada wa Mashirika ya Habari ya Kimataifa.

Wednesday, March 02, 2016

MAGUFULI NA MUSEVENI WAKUBALIANA UJENZI WA BOMBA LA KUSAFIRISHIA MAFUTA IKULU NDOGO JIJINI ARUSHA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amekutana na kufanya Mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Tanga Tanzania hadi nchini Uganda.
Rais Museveni amemtembelea Rais Magufuli katika Ikulu Ndogo ya Arusha jana jioni mara baada ya kuwasili hapa nchini akitokea nchini Uganda, ambapo hapo leo atahudhuria mkutano mkuu wa 17 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Baada ya wawili hawa kufanya mazungumzo ya faragha, Rais Magufuli amesema wamekubaliana kutekeleza mradi huo wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanga hadi Uganda kwa manufaa ya nchi zote mbili na nchi nyingine za Afrika Mashariki, litakuwa na urefu wa kilometa 1,120 na kwamba mradi huo utazalisha ajira za watu zaidi ya 15,000.
Rais Magufuli ameongeza kuwa pamoja na kujengwa kwa bomba la mafuta, pia wamezungumzia kuongeza biashara ndani ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, kujenga viwanda na kuzalisha ajira zaidi kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji mali.
Ikulu ndogo Arusha.

Rais Magufuli amesema katika mkutano huu nchi wanachama watajadili maombi ya nchi ya Sudan Kusini kupata uanachama ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa Sudan Kusini kuwa mwanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa na uwezo wa kufanya biashara katika eneo lenye takribani watu milioni 150.
Kwa upande wake Rais Yoweri Museveni pamoja na kuunga mkono yaliyosemwa na Rais Magufuli amempongeza kwa kasi yake nzuri aliyoanza nayo katika uongozi na amesema ni matumaini yake kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sasa zitakuwa katika nafasi nzuri ya kwenda kwa kasi ya Rais Magufuli katika maendeleo.

WAHUKUMIWA MIAKA 120 NA FAINI YA BILIONI 1.4

Mahakama ya hakimu mkazi Singida imewahukumu washitakiwa sita adhabu ya kutumikia jela jumla ya miaka 120 na kulipa faini ya jumla ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.4, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumiliki kinyume na sheria vipande 53 vya tembo vyenye thamani ya shilingi 149,336,000 na kosa la jingine la uwindaji.
Washitakiwa hao ni Eliud Selema Mayunga (38) mkazi na mkulima wa kijiji cha Kiombo,Ramadhani Said Biladuka (47) mkulima mkazi wa Itigi,Lenard Oscar Sunzu (31) mkazi wa kijiji cha Karangari,Pilimon Michael Kanyonga (31) mkazi wa Kitaraka Itigi,Iddi Waziri Issah Ustadh (30) mkazi wa kijiji cha Kiombo na Jimmy Charles Lyimo (39) mfanyabiashara wa Tabora Kyombo.
Mwendesha mashitaka na mwanasheria wa serikali Petrida Mutta alidai mbele ya hakimu mfawidhi mwandamizi wa mahakama hiyo, Jocye Minde kuwa mnamo Machi, 31 mwaka 2014, muda usiojulikana washitakiwa kwa pamoja walikamatwa wakiwa wamehifadhi na kumiki vipande hivyo 53 vya meno ya tembo nyumbani kwa mshitakiwa Issa Ustadh, huku wakijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo mwanasheria wa serikali, Mutta aliiomba mahakama hiyo kuwapa washitakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwao.
“Mheshimiwa kwa sasa tunaendelea kusikia na kuona vitendo vya uwindaji na biashara za nyara za serikali vikiendelea kushamiri, vitendo hivi haviwezi kufumbiwa macho kwa sababu vikifumbiwa macho, fahari ya nchi hii ya wanyama pori itatoweka naiomba mahakama yako itoe adhabu kali si tu iwe fundisho kwa washitakiwa mbali iweze kuwaonya na watu wengine wanaotaka kujihusisha na uwindaji na biashara haramu ya nyara za serikali,” alisema mwanasheria huyo wa serikali.
Kwa upande wa washitakiwa ambao wakili wao Mr. Josephat Raphael Wawa hakuwepo wakati hukumu hiyo inatolewa kila mmoja kwa nafasi yake aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu.
Akitoa hukumu hiyo iliyosikilizwa na umati mkubwa wa wananchi, hakimu Minde alisema upande wa jamhuri imethibitisha bila kuacha shaka yoyote kwamba washitakiwa wanayo hatia kwa makosa yote mawili.
“Kwa kosa la kwanza la kumiliki kinyume na sheria vipande 53 vya meno ya tembo,kila mmoja wenu atatumikia jela miaka 20 na kila mmoja wenu, atalipa faini ya shilingi 248,893,333.30 kwa kosa la pili la kujihusisha na uwindaji haramu,kila mmoja wenu,” alisema hakimu. CHANZO: mjengwablog.com



RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI KAGUTA MUSEVENI


CLINTON NA TRUMP WAONGOZA

Clinton ameshinda majimbo matano
***
Mgombea wa Democratic Hillary Clinton na mgombea wa Republican Donald Trump wamechukua uongozi wa mapema katika mchujo wa kuteua wagombea urais Marekani katika vyama vyao.
Wagombea wote wawili wameshinda majimbo ya Alabama, Georgia, Tennessee na Virginia.
Bw Trump hata hivyo ameshindwa na Seneta Ted Cruz majimbo ya Texas na Oklahoma.
Mgombea wa Democratic Bernie Sanders naye ameshinda kwake nyumbani katika jimbo la Vermont na pia katika jimbo la Oklahoma.
Donald Trump anaongoza chama cha Republican
Mchujo wa Jumanne Kuu hushuhudia majimbo 11 yakifanya mchujo kwa pamoja huku maandalizi ya uchaguzi mkuu tarehe 8 Novemba yakiendelea kushika kasi.
MOJA KWA MOJA: Mchujo wa Jumanne Kuu Marekani
Bi Hillary Clinton, aliyekuwa wakati mmoja waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, pamoja na mfanyabiashara tajiri kutoka New York Donald Trump walipigiwa upatu kushinda majimbo mengi Jumanne Kuu.
Bi Clinton pia ameshinda Arkansas na Texas, naye Bw Trump akashinda Massachusetts.
Utafiti wa maoni ya paada ya kura unaonyesha Trump na gavana wa Ohio John Kasich wakikabiliana vikali katika mchujo wa chama cha Republican jimbo la Vermont.
Bi Clinton na Bw Sanders pia wanakabiliana vikali katika jimbo la Massachusetts, kaskazini mashariki mwa Marekani.
Matokeo kutoka majimbo yaliyosalia yanatarajiwa kutolea katika saa chache zijazo. CHANZO: BBC