DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, November 27, 2014

11 WAFARIKI AJALINI TANGA LEO ASUBUHI


WATU 11 wanadaiwa kufariki dunia huku wengine wakijeruhiwa katika ajali mbaya eneo la Mkanyageni mkoani Tanga baada ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 410 BJD kugongana na Scania namba T 605 ABJ asubuhi hii.
Katika ajali hiyo, Coaster lilikuwa likitoka mkoani Tanga kwenda Lushoto na madereva wa magari yote mawili hawajulikani walipo baada ya ajali.
Miili ya marehemu katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza, Tanga.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. AMEN

DANGOTE AKAGUA UJENZI WA KIWANDA CHAKE CHA SARUJI MTWARA KWA MARA YA PILI

Alhaji Aliko Dangote kutoka Nigeria, akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara leo.
Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Manjanbu akimlaki Alhaji Dangote.
Dangote akikaribishwa na viongozi wa kampuni ya Dil & Sinoma alipowasili eneo la Kiwanda cha simenti cha Dangote.
Alhaji Dangote akiwa na maofisa wake  katika kikao na viongozi wa kampuni inayojenga kiwanda hicho ya Dil & Sinoma kwa ajili ya kupewa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kitakuwa cha tatu kwa ukubwa Afrika.
Waandishi wa habari wakimhoji Dangote kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho.
Alhaji Dangote akiwa kwenye msafara wa magari akikagua maendeleo ya ujenzi ya kiwanda cha saruji Mtwara.




Alhaji Dangote akisindikizwa kwenda kupanda ndege kwenda nchini Ethiopia kuendelea na ziara yake.
Ofisa Mnadhimu wa Poilisi Mkoa wa Mtwara, George Salala akiagana na Alhaji Dangote.
Alhaji Dangote akipanda ndege tayari kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Ndege iliyombeba Alhaji Dangote ikipaa.

KINANA AISASAMBUA CHADEMA NEWALA - NANGWANDA SIJAONA ATUA CCM

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Newala Kepteni Goerge Mkuchika wakati wa mapokezi wilayani Newala.
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akiwa amekabidhi kadi yake na ya mkewe kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona  akitangaza rasmi kurejea CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama Newala.
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akivua nguo za Chadema mbele ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchagua korosho na kuzitenga kutokana na ubora wa madaraja kwenye kiwanda cha Micronix kilichopo Newala mkoani Mtwara.
 Wafanyakazi wakibangua korosho kwenye kiwanda cha Micronix Newala ambacho kilitembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama mkoani Mtwara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia)akishiriki kusuka nondo pamoja na mbunge wa Jimbo la Newala Kepteni George Mkuchika kwenye ujenzi wa tenk la maji Kilidu wilayani Newala mkoa wa Mtwara.

Tuesday, November 25, 2014

MKURUGENZI WA DOMLAND BLOG AAGA UKAPERA

Mkurugenzi Mkuu wa Ciwanje Junior Enterprises Co. Ltd na mmiliki wa DomLand Blog, Benton Nollo (kushoto) akiwa na furaha pamoja na mkewe kipenzi Maria Gabriel Kassimba muda mfupi baada ya kufunga ndoa Novemba 21, 2014. Misa Takatifu ya Sakramenti ya Ndoa hiyo ilifanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Paulo wa Msalaba, Dodoma mjini. Picha na Mroki Mroki.
Mkurugenzi Mkuu wa Ciwanje Junior Enterprises Co. Ltd na mmiliki wa DomLand Blog, Benton Nollo (katikati) akiwa pamoja na mkewe Maria Kassimba kwenye tafrija ya ndoa yao iliyofanyika Novemba 21, 2014 kwenye ukumbi wa Lands Mark Kilimani Dodoma. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Fatma Ally. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Bahi, Rachel Chuwa akifuatiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bahi, Salome Singano.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatma Ally (kushoto) wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali katika hafra hiyo.
 

ZITO ASEMA MAISHA YAKE YAPO HATARINI

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe.

Siku moja kabla ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwasilisha bungeni, ripoti ya uchunguzi wa IPTL kuhusu ufisadi katika akaunti ya Escrow, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe amesema amekuwa akipata vitisho ili kuzuia ripoti hiyo.
Akizungumza jana, Zitto alisema pamoja na vitisho hivyo haogopi kwa kuwa maisha yake ameshayaweka nadhiri siku nyingi.
"Kuna kundi la wahuni kutoka Musoma limeletwa Dodoma likiongozwa na mtu (jina tunalihifadhi) mwenye rekodi ya ujambazi. Hivi sasa anashikiliwa na polisi kwa kukutwa na nyaraka zilizoibwa Ofisi ya Bunge. Usalama wa wajumbe wote wa PAC upo shakani," alisema Zitto.

Aliongeza kuwa kuna vipeperushi vimesambazwa mjini Dodoma kumkashifu lakini havitamsumbua kwa kuwa yeye anataka ukweli ujulikane.
Baadhi ya wabunge jana walionekana na kitabu kilichoandikwa 'mjue Zitto Kabwe kama mtetezi wa wanyonge,' lakini ndani yake kikiwa na mambo ya kumchafua mbunge huyo.
Vitabu hivyo vinaelezwa kusambazwa kwa wabunge katika nyumba zao vikilenga kuonyesha kwamba Zitto hafai kusimamia PAC ambayo hivi sasa inashughulikia escrow.
Wakati Zitto akisema hayo, suala hilo la vitisho jana pia liliibuka bungeni baada ya Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed kueleza kuwa hali ni tete kuhusu usalama wa wabunge kutokana na escrow.
Akiuliza swali la nyongeza, Mohamed alisema usalama wa wabunge uko shakani kuanzia maeneo wanayofanyia kazi na makazi yao na hasa kipindi hiki tangu kuanza kwa sakata la escrow.
"Je, nini tamko la Serikali juu ya ulinzi na usalama wa wabunge katika maeneo ya kazi, pia katika maeneo yao ambayo wanaishi?" alihoji.
Kabla ya majibu kutolewa na Serikali, Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye jana alianza kuongoza vikao baada ya safari yake nje ya nchi, aliingilia kati akisema ofisi yake inakusudia kujenga kijiji cha wabunge ambako watalindwa kwa pamoja.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba alisema Serikali inafanya tathmini ya vitisho vyote vya viongozi nchini wakiwamo wabunge ili kuhakikisha wanakuwa salama.

TUZO ZA FILAMU TANZANIA ZAZINDULIWA RASMI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, akiongea neno wakati wa uzinduzi wa Tuzo za filamu Tanzania chini ya Shirikisho la Filamu Tanzania.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba akielezea jambo katika hafla za uzinduzi wa Tuzo za Filamu Tanzania zilizofanyia mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Lulu akipozi kwa picha katika uzinduzi huo. 
Kelvin akiwa katika zulia jekundu la uzinduzi huo.  
Wasanii wakipiga picha ya pamoja.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa tasnia ya filamu nchini.

Wasanii wa Filamu Tanzania wakiwa katika furaha baada ya kuzinduliwa kwa Tuzo.

TARATIBU ZA TIBA KWA RAIS WA TANZANIA MHE. PROF. JAKAYA KIKWETE MAREKANI ZAKAMILIKA

Taratibu za matibabu kwa Rais Jakaya Kikwete zimekamilika jana (Jumatatu) Novemba 24, 2014 baada ya madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo mjini  Baltimore, Jimbo la Maryland nchini Marekani kufanya uthibitisho wa mwisho kuhusu afya yake. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Kiongozi huyo wa ngazi ya juu nchini Tanzania aliondoka Novemba 06, 2014 kwenda Marekani kwa ajili ya kufanyiwa matibabu na Novemba 08, 2014 alifanyiwa upasuaji wa tezi dume. Aidha, Rais kikwete anatarajia kurejea nchini Novemba 29, 2014.

Thursday, November 13, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MAZISHI YA RAIS SATA NCHINI ZAMBIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata Ikulu mjini Lusaka Zambia Novemba 11, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal wa kwanza (kushoto) akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Rupia Banda, Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Msumbiji Mhe. Ermando Guebuza na Kaimu Rais wa Zambia Dkt. Guy Scott kwenye Misa Maalum ya kuaga mwili wa Rais Michael Sata iliyofanyika Novemba 11, 2014 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha Tawala cha PF Mhe. A.B. Chikwanda kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa wakati mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata yaliyofanyika Novemba 11, 2014 kwenye uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais mstaafu wa kwanza Zambia Dkt. Keneth Kaunda mara baada ya kumalizika maziko ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika Novemba 11, 2014 mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais mstaafu wa Zambia Mhe. Ruphia Banda baada ya kumalizika mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika juzi Novemba 11,2014. katikati Rais mstaafu wa kwanza wa Zambia Dkt. Keneth Kaunda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu cha maombolezo ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika Novemba 11, 2014. (Picha na Ofisi ya Makamu Rais)

RAIS KIKWETE ATOKA HOSPITALI JANA

Rais Prof. Jakaya Mrisho Kikwete  akisindikizwa na Daktari Bingwa Edward Schaeffer wa Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita. Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
 

Rais Prof. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita. Picha na Freddy Maro.

YASOMEKAVYO MAGAZETI ALHAMISI YA LEO