DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, November 03, 2014

DKT. BILLAL AFUNGA KONGAMANO LA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA SUMBAWANGA MJINI MKOANI RUKWA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa Ziwa Tanganyika lililojumuisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma hivi karibuni. Kongamano hilo limefungwa Novemba 01, 2014  katika Uwanja wa Nelson Mandela  Sumbawanga mjini, Mkoani Rukwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi na tano kwa wajasiriamali wadogo wadogo wa Sumbawanga kwenye Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa ziwa Tanganyika linalojumuisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya ambaye Mkoa wake ndio Mwenyeji wa Kongamano hilo kwa mwaka 2014. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi  kwa wajasiriamali wa Halmashauri ya Mji Mpanda kwenye Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa Ziwa Tanganyika linalojumuisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia mashati ya vitenge alipotembelea banda la Mkoa wa Katavi, maonesho ambayo yaliandaliwa wakati wa Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa Ziwa Tanganyika linalojumuisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Col. Mstaafu Issa Machibya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ndizi za aina mbalimbali alipotembelea banda la Mkoa wa Kigoma kwenye maonesho wakati wa Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa Ziwa Tanganyika linalojumuisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Picha zote na Ofisi ya Makamu Rais.

No comments:

Post a Comment