Taratibu za matibabu kwa Rais Jakaya Kikwete zimekamilika jana (Jumatatu) Novemba 24, 2014 baada ya madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo mjini Baltimore, Jimbo la Maryland nchini Marekani kufanya uthibitisho wa mwisho kuhusu afya yake. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Kiongozi huyo wa ngazi ya juu nchini Tanzania aliondoka Novemba 06, 2014 kwenda Marekani kwa ajili ya kufanyiwa matibabu na Novemba 08, 2014 alifanyiwa upasuaji wa tezi dume. Aidha, Rais kikwete anatarajia kurejea nchini Novemba 29, 2014. |
No comments:
Post a Comment