WATU 11
wanadaiwa kufariki dunia huku wengine wakijeruhiwa katika ajali mbaya
eneo la Mkanyageni mkoani Tanga baada ya gari aina ya Toyota Coaster
yenye namba za usajili T 410 BJD kugongana na Scania namba T 605 ABJ
asubuhi hii.
Katika
ajali hiyo, Coaster lilikuwa likitoka mkoani Tanga kwenda Lushoto na
madereva wa magari yote mawili hawajulikani walipo baada ya ajali.
Miili ya marehemu katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza, Tanga.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. AMEN |
No comments:
Post a Comment