Mjini Derna, kundi la Is limeshika hatamu
Wanaharakati
watatu wa kisiasa nchini Libya wamechinjwa baada ya kuandika katika
mitandao ya kijamii juu ya maisha ya chini ya utawala wa Dola ya Kiislam. Miili yao ilipatikana mapema wiki hii mashariki mwa mji wa Derna
karibu na Benghazi.
Tukio
hilo lilianzia kwa wanaharakati hao kutekwa mapema mwezi huu. Mji huo wa
Derna uko chini ya mamlaka ya kikundi cha Dola ya Kiislam tangu mwaka
2012 ambacho kimekiri kuwa sehemu ya kundi la IS.
Mnamo
mwezi Augosti mwaka huu katika video ilooneshwa katika mitandao ya
kijamii ilionesha mwanamume mmoja akipigwa risasi na kufa hadharani
katika viwanja vya mpira mjini Derna.
Siku za hivi karibuni kuna picha iloachiliwa mitandaoni ikionesha kikundi cha kijamii kinachojiita Mahakama ya Kiislam. Picha na habari hii ni kwa hisani ya BBC |
No comments:
Post a Comment