Wafanyakazi wa afya huko Sierra Leone
Serikali
ya Sierra Leone imesema italipa dola elfu tano za kimarekani kama fidia
kwa familia ya kila mfanyakazi wa afya ambaye amefariki baada ya
kuambukizwa Ebola wakati akihudumia wagonjwa wa Ebola.
Kituo cha
taifa cha kupambana na Ebola nchini humo kimesema fidia hiyo ya mara
moja pia kwa ndugu wa wafanyakazi wa afya zaidi mia moja ambao wamekufa
kwa ugonjwa huo hapo awali.
Virusi
vya ugonjwa huo vimekuwa vikisambaa kwa kasi nchini Sierra Leone ambapo
katika muda wa siku tatu zilizopita zaidi ya watu mia tatu wamegundulika
kuambukizwa ugonjwa huo.
Mwezi
uliopita serikali ya Guinea nayo ilisema ingeanza kulipa dola elfu kumi
kwa kila familia ya mfanyakazi wa afya aliyeambukizwa Ebola wakati
akitekeleza majukumu yake.
Wakati
huo huo Mwakilishi wa Umoja wa mataifa kuhusu haki ya chakula Hilal
Elver amesema zaidi ya watu milioni moja nchini Afrika ya Kati
wanahitaji chakula cha msaada kutokana upungufu wa chakula uliotokana na
maambikizi wa virusi vya Ebola. Picha na habari hii ni kwa hisani ya BBC. |
No comments:
Post a Comment