JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MKUTANO WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAHERE 4 – 28 NOVEMBA, 2014 – DODOMA
Kufuatia
uwepo wa Bunge Maalum la Katiba lililomalizika mwezi Oktoba, Mkutano wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Kumi na Sita na wa Kumi na
Saba ilipangwa kufanyika kwa pamoja kuanzia tarehe 4 – 28 Novemba, 2014
mjini Dodoma.
Kazi
zitakazofanyika katika mikutano hiyo ni pamoja na Bunge kukaa kama
Kamati ya Mipango kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 94(1) na kupokea,
kujadili na kutoa maoni na ushauri kuhusu bajeti ya serikali, vyanzo vya
mapato pamoja na mapendekezo ya utekelezaji wake.Aidha kutakuwa na
kusomwa kwa mara ya pili na hatua zake zote kwa miswada ya Sheria ya
Serikali ambayo ilikwishasomwa kwa mara ya kwanza katika mikutano
iliyotangulia; Muswada Binafsi wa Mbunge na Muswada Binafsi wa Kamati
kama ifuatavyo:
A. Miswada ya Sheria ya Serikali
i. Muswada ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani wa Mwaka 2014. [The Value Added Tax Bill, 2014]
ii. Muswada wa Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2013. [The Statistics Bill, 2013].
iii. Administration Bill, 2014]
iv.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya
Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2014 [The Public Private Partnership
(Amendment) Bill, 2014] na,
v. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa Mwaka 2014. [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2014]
B. Muswada Binafsi wa Mbunge
Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana wa Mwaka 2013. [The Youth Council Bill, 2013]
C. Muswada Binafsi wa Kamati
Muswada wa Sheria ya Bajeti wa Mwaka 2014. [The Budget Bill, 2014].
Aidha,
Bunge litapokea taarifa ya Kamati Teule iliyoundwa tarehe 1/11/2013 ili
kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi,
kilimo, mifugo, maji na uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika
matumizi ya ardhi.
Pamoja na mambo mengine, Bunge pia litajadili maazimio matatu ambayo ni:
i. Azimio
la kuridhia Itifaki ya Afrika Mashariki Kuhusu Ushirikiano katika
Masuala ya Kiulizi. [The East African Protocol on Cooperation in Defence
Affairs].
ii.
Azimio la Bunge kuhusu mapendekezo ya kuridhia makubaliano ya msingi ya
Ushirikiano katika Bonde la Mto Nile, [Agreement on the Nile River Basin
Co-operative Framework – CFA]; na
iii.
Azimio la kuridhia Itifaki ya Uzuiaji wa Vitendo Haramu dhidi ya Usalama
wa Miundombinu ya kudumu iliyojengwa chini ya Bahari katika mwambao wa
Bara ya mwaka 1988.[The Protocol for the Suppression of Unlawful Acts
against the Safety of Fixed Platforms located on the Continental Shelf –
SUA, 1988].
Aidha,
kutakuwa na maswali ya kawaida kwa mujibu wa kanuni ya 39(1) ambapo kwa
mikutano hii miwili yakuwa 265 na maswali kwa Waziri Mkuu kwa mujibu wa
kanuni ya 38(1).
Mwisho
Waheshimiwa Wabunge wakiwa Dodoma watapata fursa ya kushiriki semina
mbalimbali za kujenga uwezo katika nyanja za kilimo na usalama wa
chakula; faida za ushirikiano katika Bonde la Mto Nile; na umuhimu wa
kupima/kuchunguza afya mara kwa mara.
Ratiba ya Mkutano itatolewa mara baada ya kikao cha Kamati ya Uongozi kitakachofanyika tarehe 4 Novemba 2014, Dodoma.
Imetolewa na Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam,
30 Oktoba 2014
|
No comments:
Post a Comment