Kocha wa zamani wa timu ya Manchester United, David Moyes ametajwa kuwa meneja mpya wa timu ya Hispania, Real Sociedad.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 51, hii ni kazi yake ya kwanza baada ya kutimuliwa kwenye klabu cha Man Utd mwezi wa nne mwaka huu,
Moyes
anachukua nafasi ya Jagoba Arrasate ambaye pia ametimuliwa na Sociedad
baada ya matokeo mabaya na kusababisha timu hiyo kuangukia nafasi ya 15
katika ligi kuu nchini humo, maarufu kama La Liga.
Mkataba
wa Moyes na Real Sociedad ni mpaka Juni mwaka 2016 na kwama mara ya
kwanza ataonekana katika mechi ya Deportivo Novemba 22 mwaka huu. |
No comments:
Post a Comment