DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, November 12, 2014

TCRA YATOA MAFUNZO KWA WAMILIKI WA BLOGS (BLOGGERS) TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John Nkoma akitoa hotuba yake wakati wa ufungumzi wa Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wenye lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini, uliofanyika jana katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Andrew Kisaka akitoa Mada katika  Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wenye lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali katika wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),Assah Mwambene akitoa hotuba yake wakati  akifunga Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania uliokuwa na lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini. Mafunzo hayo yalifanyika jana katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.
Moja ya Mada zilizowasilishwa jana kwenye Mkutano huo.

                    
 Sehemu ya Wanablog waliohudhuria Mkutano huo uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Othman Michuzi.

No comments:

Post a Comment