Hatma
ya nani atakuwa mwenyeji wa kombe la mataifa ya Africa 2015 maarufu
kama Africa Cup of Nations lazima ajulikane, kwani kamati ya shirikisho
la vilabu vya soka barani Africa imekutana kujadili juu ya suala hili .
Morocco
ndiye aliyekuwa anapewa nafasi kubwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo
kuanzia tarehe 17 mwezi wa kwanza hadi mwezi wa pili tarehe 8, lakini
kuna kila dalili Morocco inataka kuahirisha michuano hiyo kwa hofu dhidi
ya ugonjwa hatari wa Ebola kuwa utaingia nchini humo.
Leo ndiyo
leo, leo inapaswa kuwa siku ya kuamua kati ya Morocco na bodi ya
shirikisho la mpira wa miguu barani Africa CAF, ile sintofahamu baina
yao inatatuliwa.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita waziri wa michezo wa Morocco,alisimama na kuongea kwa
kifupi yakwamba hawataweza kuwa mwenyeji wa michuano hiyo na badala
yake wasikilizwe ombi lao la kuahirishwa kwa michuano hiyo mpaka mwaka
wa 2016.
Wakati
hayo yakijiri CAF wametoa msimamo wao ya kuwa tarehe ya kuanza kwa
michuano hiyo haitabadilika,sasa swali linakuja je CAF wana nchi
nyingine iliyotayari kupokea michuano hiyo na kuwa mwenyeji? Ilhali
imebakia wiki kumi tu? Na kama inawezekana basi itakuwa ni kati ya nchi
zilizokuwa wenyeji wa michuano hiyo miaka ya karibuni,ambayo CAF ina
uhakika na miundo mbinu yake na uwanja ulio tayari ndani yake.
Mnamo
mwaka 2013, mwenyeji wa michuano hiyo ilikuwa ni Africa Kusini ambayo
tayari imekwishatoa msimamo wake kuwa wala wasiitie mawazoni kuwa wao
ndo kimbilio la kunusuru michuano ya mwaka huu.
Kwa upande wao CAF sasa wanatarajiwa kutoa tamko lao la mwisho juu ya suala hili, haraka iwezekanavyo. |
No comments:
Post a Comment