DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, February 08, 2016

HENRY AHOJI UWEZO WA ARSENAL MBIO ZA UBINGWA

Mchezaji nguli wa zamani wa klabu za Arsenal na Barcelona, mfaransa Thierry Henry ameuliza uwezo ‘mentality’ wa Arsenal katika harakati za kuwania ubingwa wa ligi kuu nchini England,  baada ya kuukosa kwa zaidi ya miaka kumi hivi sasa.
Baada ya klabu ya Arsenal jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 nyumbani kwa Bournemouth mabao ya Oxlade Chamberlain na Mesut Ozil, kocha wa Arsenal mfaransa Arsene Wenger amejinasibu kuwa Arsenal bado wako katika mbio za ubingwa msimu huu, huku akiwataja Leicester kuwa wako katika nafasi nzuri zaidi katika mbio hizo.
Leicester City wamewafunga Liverpool na Manchester City ndani ya wiki moja na sasa wamekaa kileleni kwa tofauti ya points tano wakizipita Tottenham Hotspur, Arsenal na Manchester City.
Lakini Thierry Henry anasema klabu yake hiyo ya zamani haina mentality nzuri katika mbio hizo, huku akikumbushia mechi dhidi ya Chelsea na kudai kuwa ni mechi unahitaji kupata matokeo kama kweli unataka ubingwa.  Thierry pia amesema kuwa Leicester sasa wanaonekana kukomaa zaidi na anaamini lolote linaweza kutokea huku akiamini Leicester wana nafasi kubwa ya kuutwaa ubingwa huo wa England.
Kocha wa Leicester mara kadhaa msimu huu, amekua akiondoa imani hiyo kuwa timu yake iko katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa huo huku akisema kuwa wao hivi sasa wanaangalia zaidi mechi iliyopo mbele yao zaidi ya kuutizama msimu wote.

No comments:

Post a Comment