DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, February 25, 2014

WANAWAKE WAOMBA KUPEWA KIPAUMBELE NA WAMILIKI WA MAENEO YA BIASHARA NCHINI


Mwenyekiti wa Tancraft, Elihaika Mrema akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa jumuiya kubwa za wafanyabiashara na pamoja na serikali kuwaunga mkono wajasirimali wanawake nchini, Kushoto ni Esther Kasenga Msaidizi wa Katibu, Kulia Mweka hazina wa Chama cha Tancraft, Bi.Louise Judicate na Wapili kulia ni Katibu wa Tancraft, Bi. Vicky Shayo.


Baadhi ya Wajasiriamali wa DAR FREE MARKET wakionyesha bidhaa zao. Watanzania tuwaunge mkono wenzetu!

Mwandishi wa kituo cha Televisheni cha ITV, Fatma Almasi, akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na Batiki. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Tancraft, Elihaika Mrema na wa tatu kulia ni Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Televisheni cha Channel Ten Bw. Salum Mkambala.

Fatuma Amour kutoka kampuni ya Famour Designer akionyesha moja ya kazi za mikono yake.

Hii ni moja ya zawadi ya kikombe kwa Chama cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TANCFRAFT) walichowahi kupata kwa kuonyesha bidhaa zenye ubora wa kimataifa.(Picha kwa hisani ya mrokim blog)

UEFA: MAN UTD USO KWA USO NA OLYMPIAKOS MABINGWA WA SOKA NCHINI UGIRIKI



NYALANDU ATANGAZA MABADILIKO YA UONGOZI IDARA YA WANYAMAPORI

Leo, TAREHE 24 Februari, 2014 Natangaza kuubadili uongozi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya maliasili na Utalii kama ifuatavyo: 

Ninamuondoa Profesa Alexander Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii.  Nachukua hatua hii kutokana na kutokuridhishwa kwangu na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini.  

Aidha, hatua hii ni utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotolewa tarehe 22 Disemba, 2013, lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza. Utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul Sarakilya kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wziara ya Maliasili na Utalii kuanzia sasa. Aidha, ninamuondoka Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dr. Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo. 

Hali kadhalika, ninamteua Bwana Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji – Ujangili na anachukua nafasi ya anayeenda kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori.Vilevile, Bibi Nebbo Mwina anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu, na Bwana Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori. Pamoja na Kitengo cha Uzuiaji – Ujangili nilichokitaja awali, hivi ni vitengo vya Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utafiti. 

Nawaagiza kwamba Wakurugenzi na Wakuu wote wa kila Idara, kila Shirika, na Taasisi zote ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutengeneza viashiria muhimu vya utendaji kazi (Key Performance Indicators) nakukabidhi kwangu ndani ya siku 30 zijazo.  Viashiria hivi ni hatua ya kufanikisha yafuatavyo, 1)  Malengo ya wizara, 2)  Uwajibikaji, 3) Uwazina 4) Ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku.  Ni sharti tutekeleze mikakati ya wizara katika mifumo inayopimika, tuweze kujipima natuweze kupimwa, natutumikie Taifa kwa uadilifu.

Kwa mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo mimi mwenyewe, Lazaro Nyalandu, atapaswa kuzingatia na kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Mwenendo (Code of Conduct) ambazo zitapendekezwa na kupitishwa na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara.  Baraza hili liwe limeitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara kabla ya mwisho ya mwezi ujao.  Azma ya kanuni hizi ni kuwa na misingi bora ya utumishi, uwajibikaji, utu, usawa na haki katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku. 
Mungu ibariki Tanzania.
Asante.

Lazaro S. Nyalandu (MB)
Wizara ya Maliasili na Utalii
24/02/2014