Askofu mstaafu wa Cape Town, Desmond Tutu, amemsihi Rais
Museveni wa Uganda (pichani) asitie saini mswada uliozua sintofahamu
juu ya wapenzi wa jinsia moja nchini humo. Akofu Tutu, aliyewahi kupata tuzo ya
amani ya Nobel, alisema amevunjika moyo kuwa Rais Yoweri Museveni anaonesha
kubadilisha msimamo wake, kwa vile awali alisema kuwa hataruhusu mswada huo
kuwa sheria. Desmond Tutu alisema haistahiki kuwa na ubaguzi kama huo, na
ametoa mifano ya mfumo wa zamani wa ubaguzi wa rangi uliokuwepo Afrika Kusini
na ule wa Wa-Nazi wa Ujerumani. Alisema kuwa hiyo ni mifano mibaya kabisa
duniani. Awali mswada wa Uganda ulipendekeza kifo kwa vitendo vya kulawiti na
baadae kubadilishwa kuwa adhabu ya kifungo.
|
No comments:
Post a Comment