DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, February 24, 2014

RAIS WA UKRAINE ALIYEONDOLEWA MADARAKANI VICTOR YANUKOVYCH KUKAMATWA

Ukraine imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais aliyeondolewa madarakani, Victor Yanukovych. Hatua hiyo imetangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa mpito wa nchi hiyo, Arsen Avakov katika ukurasa wake wa Facebook kwa kusema kuwa kesi dhidi ya Yanukovych na maafisa wengine imefunguliwa kuhusu mauaji ya makubwa ya watu. Jumamosi iliyopita Wabunge walipiga kura ya kumuondoa Yanukovych baada ya maandamano ya miezi kadhaa yaliyojitokeza baada ya kupinga kujiunga na Umoja wa Ulaya. Machafuko yaliyotokana na maandamano hayo yalisababisha watu kadhaa kupoteza maisha juma lililopita. Avakov amesema Yanukovych alionekana mjini Balaklava siku ya jumapili, lakini mpaka sasa hajulikani mahali alipo.

No comments:

Post a Comment