DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, February 18, 2014

RUBANI MSAIDIZI NDIYE ALIYETEKA NYARA NDEGE YA ABIRIA YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETHIOPIA

Hii ndiyo ndege iliyotekwa nyara na Rubani Msaidizi wa shirika la ndege la Ethiopia mara baada ya kuchukua usukani wa ndege hiyo kufuatia rubani wake kwenda msalani. Tukio hilo lilitokea wakati ndege hiyo aina ya Boeing 767-300 ilipokuwa ikipaa katika anga ya Sudan kuelekea Rome Italia ambapo aliibadilishia mkondo na kuielekeza Uswisi na kutua katika uwanja wa ndege wa Geneva. Shirika hilo la ndege limebainisha kuwa abiria wote 200 waliokuwa katika ndege hiyo wapo salama. Ripoti ya idara inayosimamia usafiri wa ndege ya Uswisi imesema kuwa rubani huyo msaidizi aliomba uraia kabla ya kutua na baada ya kutua alijisalimisha kwa maafisa wa usalama waliokuwa wameizingira ndege hiyo ambapo polisi walimtia mbaroni mara moja. (chanzo BBC Swahili).

No comments:

Post a Comment