DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, February 24, 2014

MAPENZI YA JINSIA MOJA YAPIGWA STOP NCHINI UGANDA


Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini mswada wenye utata unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Rais Museveni alitia saini mswada huo nyumbani kwake katika hafla iliyoshuhudiwa na Maafisa Wakuu wa Serikali pamoja na Wandishi wa Habari. Mswada huo ambao sasa utakuwa sheria, unatoa adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wale watakaopatikana na hatia kwa mara ya kwanza. Adhabu ya maisha jela itatolea kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja zaidi ya mara moja kati ya watu wawili waliokubaliana kufanya hivyo. Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi. Mswada huo umepigiwa debe sana nchini Uganda, lakini Mashirika ya Kimataifa ya kutetea Haki za Binadamu yameulaani vikali. (Ni kwa hisani ya BBC Swahili).

No comments:

Post a Comment