DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, September 30, 2014

C. RONALDO APIGA HAT-TRICK YA 25 AKIWA NA REAL MADRID

Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wakishangilia ushindi wao wa 5-1 jana dhidi ya Elche.

NYOTA Cristiano Ronaldo amepiga hat-trick yake ya 25 akiwa na Real Madrid kikosi cha Carlo Ancelotti kikifikisha mabao 18 katika mechi tatu kufuatia ushindi wa 5-1 dhidi ya Elche katika La Liga. Ronaldo alifikisha mabao nane ndani ya wiki na baada ya mechi alipoulizwa kama bado ana furaha Madrid alisema. "Mambo yanakwenda vizuri na zaidi binafasi na timu inafunga mabao, inashinda mechi na kucheza vizuri.'

Wednesday, September 24, 2014

ZANZIBAR JANA YAADHIMISHA MIAKA 50 YA EIMU BILA MALIPO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Walimu na Wanafunzi katika Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanafunzi waliopita mbele ya jukwaa la viongozi katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar wakati wa sherehe za kilele cha miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe Msaidizi Afisa Elimu Mkoa wa Kaskazini Unguja Maulid Nafasi Juma wakati wa Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja jana.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

CHENGE AKABIDHI RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA MWENYEKITI BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO HII


Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba Mhe. Andrew Chenge akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe. Samuel Sitta Rasimu ya Katiba inayopendekezwa wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi cha Bunge leo. Kamati ya Uandishi imemaliza kazi ya kuandaa Rasimu hiyo na inatarajiwa kusomwa Bungeni kesho.

LIVERPOOL YABANWA MBAVU...YANUSURIKIA KWENYE MATUTA

Mario Balotelli akipambana jana Anfield

KLABU ya Liverpool imeifunga Middlesbrough kwa penalti 14-13 katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Anfield. Kinda Jordan Rossiter alianza kuwafungia Wekundu hao baada ya kupewa nafasi ya kwanza kuchezea kikosi cha kwanza, kabla ya Adam Reach kuwasawazishia wageni akimalizia pasi ya Grant Leadbitter. Mchezo huo ulihamia kwenye muda wa nyongeza kufuatia timu kumaliza zikiwa zimefungana 1-1 baada ya dakika 90.

Monday, September 15, 2014

KINANA AANZA ZIARA YA SIKU MBILI WILAYANI RUFIJI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanachama na viongozi wa CCM waliojitokeza kumpokea.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa CCM wilaya ya Rufiji Ndugu Mohamed Moyo mara baada ya kuwasili katika wilaya ya Rufiji ambako atafanya ziara ya siku mbili.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrhman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambaye pia ndie Waziri wa Afya Dk. Seif Rashidi mara baada ya kuwasili kwenye  mji wa Ikwiriri wilayani Rufiji.

MBUNGE ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGE LA MABADILIKO YA KATIBA



PICHANI ni mapokezi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliyerejea nchini kwake (Kenya) jana  baada ya kuhudhuria Mahakama ya Kimataifa ICC, iliyopo The Hague nchini Uholanzi. Kenyatta alikanusha mashtaka dhidi yake ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, zilizosababisha vifo vya watu wapatao 1,200 na wengine 600,000 kupoteza makazi. Kenyatta anakuwa rais wa kwanza aliyepo madarakani kufika katika mahakama ya ICC. Aidha, akihutubia umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza kumpokea, Kenyatta alihimiza umoja, mshikamano, kusameheana na kuyatatua matatizo ya nchi hiyo kwa pamoja. 

VAN GAAL: UNITED INALENGA TAJI LA EPL

Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amesema kuwa anapania kuirejesha Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza uwanjani Old Trafford. Kocha huyo amezungumza hivi punde baada ya Man United kusajili ushindi wake wa kwanza msimu huu. United iliilaza QPR 4-0 uwanja wa Old Trafford Jumapili iliyopita.
''Sasa nataka kurejesha taji la EPL: hapa Old Trafford ikiwa sio msimu huu basi katika mwaka wangu wa pili ama wa tatu. Isitoshe nataka mashabiki wetu washuhudie mechi z ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya.''
Van Gaal, amewahi kushinda mataji ya ligi katika misimu yake ya kwanza akiwa Barcelona na Bayern Munich, na sasa ameagizwa kumaliza katika nafasi tatu za kwanza na Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward.
Baada ya kufunga mara mbili pekee katika mechi nne za kwanza vijana wa Van Gaal, wakiongozwa na Angel Di Maria na Ander Herrera, walisajili mabao yao ya kwanza tangu watue Old trafford.
 Mabao mengine ya United yalitiwa kimiani na Wayne Rooney na Juan Mata. Van Gaal ameomba uwezo wake utathminiwe kwa jinsi atakavyo maliza msimu huu wala sio atashinda nini. Manchester United imeratibiwa kuchuana na Leicester jumapili ijayo. (Habari hii ni kwa hisani ya BBC Swahili)

WAREMBO WA SHINDANO LA MISS REDD'S TANZANIA 2014 WAJIFUA GYM KUBORESHA MIILI YAO











Warembo wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2014 jana wameingia siku ya pili ya kambi yao jijini Dar es Salaam na baada ya semina asubuhi na mapumziko ya mchana jioni hiyo walifanya mazoezi katika chumba maalum cha mazoezi 'Gym'.

MAN UNITED YAICHARAZA QPR 4-0

Mpira uliopigwa na Angel di Maria ukijaa nyavuni na kuifanya Man Utd kuongoza kwa bao 1-0 dhidi ya QPR.

  Jana ni siku njema sana kwa mashabiki na wafuasi wa timu ya Manchester United baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa bao 4-0 hadi dakika ya mwisho ya mchezo dhidi ya Queens Park Rangers (QPR) hii ni kwa mchezo wa Primer League. Mvua hiyo ya magoli ilianzishwa na nyota wake mpya Angel di Maria alipopiga mkwaju wa adhabu ndogo dakika ya 24 na baadae goli la pili kufungwa na Ander Herrera dakika ya 36 na Wayne Rooney dakika 48  kutupia la tatu na kuipeleka mampumzika ikiwa na ushindi wa 3-0.

YANGA YAIRARUA AZAM FC 3-0 NGAO YA JAMII


Kikosi kamili cha Yanga kilichoifunga Azam FC 3-0 katika mchezo wa Ngao ya jamii jana.

Kikosi cha Azam FC kilichokubali kichapo cha bado 3-0 dhidi ya Yanga jana.

Thursday, September 11, 2014

MKUTANO WA 24 WA WADAU NA WANACHAMA WA PPF WAANZA RASMI JANA, JIJINI ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha Nchini, Mhe. Mwigulu Nchemba ambaye pia ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 24 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akifungua Mkutano wa 24 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko huo unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa Mkutano wa Wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Fedha, Mh Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati wa Mkutano wa wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaoendelea katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC, Jijini Arusha.

Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 24 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF ambae pia ni Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii mara baada ya kufungua Mkutano wa 24 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba akimpongeza Meneja Masoko na Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Lulu Mengere wakati wa Mkutano wa 24 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha.



Wadau wakifuatilia Mada katika Mkutano wa 24 Wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha jana.

 Wabunge wa Chadema, Mhe. Joshua Nassari (kushoto) na Mhe. Joseph Mbilinyi (Kulia) wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF (Hayupo pichani) Mhe. William Erio wakati wa mkutano wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, Jijini Arusha.




Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mhe. William Erio (Wa Kwanza kushoto) akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Makongoro Mahanga (katikati) wakati wa mkutano wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, Jijini Arusha.

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE ZA SEKONDARI DSM

Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 4.5, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Sekondari Manispaa ya Temeke, Yasintha Kayoza kwa niaba ya shule tatu za Sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (mwenye miwani), akiangalia moja ya vitabu vya masomo ya sayansi baada ya kuvikabidhi vitabu vyenye thamani ya milioni 4.5, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 1.5, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana. Sekondari nyingine zilizokabidhiwa vitabu hivyo ni pamoja na Mvuti na Kambangwa. Kushoto ni Mwakilishi wa Shule ya Sekondari Kambangwa, Mwalimu Sueiba Mfinanga.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbagala wakifurahia vitabu vya masomo ya sayansi, baada ya Kampuni ya Airtel kupitia Mradi wake wa ‘Shule Yetu’ kukabidhi vitabu hivyo vyenye thamani ya milioni 4.5 kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana.

WASHINDI WA TUZO ZA HABARI ZA TANAPA 2013 WAENDELEA NA ZIARA YA MAFUNZO AFRIKA KUSINI

Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013. Kutoka kulia ni Vedasto Msungu (ITV), Gerald Kitabu (The Guardian), David Rwenyagira (Radio Five) na Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete katika picha ya pamoja katika ofisi za Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC) jijini Johannesburg.
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 wakifanya mahojiano ndani ya Studio za Shirika la Utangazaji la Afrika ya Kusini (SABC- Channel Afrika). Kutoka kushoto ni David Rwenyagira (Radio Five), Gerald Kitabu (The Guardian), Vedasto Msungu (ITV) na Mtayarishaji Vipindi Isaack Khomo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Wahariri Afrika Kusini Mathatha Tsedu (wa tatu kulia) akiwa pamoja na Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013. Kutoka kushoto ni Gerald Kitabu (The Guardian), Vedasto Msungu (ITV), David Rwenyagira (Radio Five) na Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete.
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 . Kutoka kulia ni David Rwenyagira (Radio Five), Vedasto Msungu (ITV), Gerald Kitabu (The Guardian) na Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete wakiwa nje ya Ofisi za Makao Makuu ya Jukwaa la Wahariri Afrika Kusini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Wahariri nchini Afrika Kusini Mathatha Tsedu (mwenye kofia) akimsikiliza kwa makini Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete wakati wa ziara ya mafunzo kwa washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 nchini humo. Baadhi ya washindi hao ni pamoja na Vedasto Msungu kutoka ITV (kulia) na Gerald Kitabu (The Guardian Newspaper).
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 wakiwa pamoja na Mhariri Mkuu wa Habari na Matukio wa Channel Afrika ya Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC) Busi Chaane (wa tatu kushoto) pamoja na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Channel Afrika ya SABC Mike Arareng (wa kwanza kulia) walipotembelea studio hizo kwa ziara ya mafunzo.