Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wakishangilia ushindi wao wa 5-1 jana dhidi ya Elche.
NYOTA Cristiano Ronaldo amepiga
hat-trick yake ya 25 akiwa na Real Madrid kikosi cha Carlo Ancelotti
kikifikisha mabao 18 katika mechi tatu kufuatia ushindi wa 5-1 dhidi ya
Elche katika La Liga. Ronaldo alifikisha mabao nane ndani ya
wiki na baada ya mechi alipoulizwa kama bado ana furaha Madrid
alisema. "Mambo yanakwenda vizuri na zaidi binafasi na timu inafunga
mabao, inashinda mechi na kucheza vizuri.' |
No comments:
Post a Comment