DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, September 11, 2014

MSHINDI WA TMT 2014, MWANAAFA MWINZAGO APOKELEWA KWA SHANGWE MTWARA

Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago akitoa Maneno ya Shukrani kwa Wakazi wa Mtwara waliojitokeza kumpokea mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara mapema jana. Vilevile alitoa Shukrani zake zote kwa Watanzania Wote kwa kumpigia kura na kumfanya aibuke mshindi wa shilingi milioni 50 za Tanzania katika fainali ya Shindano la  Kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT).
Wapenzi, Mashabiki na wana Mtwara wakiwa Nje ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara wakisubiri Kumpokea Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago kwa ajili ya kumpongeza kwa kuibuka mshindi wa shilingi milioni 50 za Kitanzania katika fainali za shindano hilo lililofanyika Mwisho wa Mwezi wa nane katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar Es Salaam.
Wakazi wa Mkoa wa Mtwara wakimpongeza mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago ambaye aliwasili jana mkoani humo mara baada ya kuibuka mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 50 za Kitanzania. Mtwara ndiko nyumbani kwa msanii huyo.

No comments:

Post a Comment