Kocha wa Manchester United Louis van Gaal
amesema kuwa anapania kuirejesha Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza uwanjani
Old Trafford. Kocha huyo amezungumza hivi punde baada ya Man United kusajili ushindi wake wa kwanza msimu huu. United iliilaza QPR 4-0 uwanja wa Old Trafford Jumapili iliyopita.
''Sasa nataka kurejesha taji la EPL: hapa Old Trafford ikiwa sio msimu huu basi katika mwaka wangu wa pili ama wa tatu. Isitoshe nataka mashabiki wetu washuhudie mechi z ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya.''
Van Gaal, amewahi kushinda mataji ya ligi katika misimu yake ya kwanza
akiwa Barcelona na Bayern Munich, na sasa ameagizwa kumaliza katika
nafasi tatu za kwanza na Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward.
Baada
ya kufunga mara mbili pekee katika mechi nne za kwanza vijana wa Van
Gaal, wakiongozwa na Angel Di Maria na Ander Herrera, walisajili mabao
yao ya kwanza tangu watue Old trafford.
Mabao mengine ya United yalitiwa kimiani na Wayne Rooney na Juan Mata. Van Gaal ameomba uwezo wake utathminiwe kwa jinsi atakavyo maliza msimu huu wala sio atashinda nini. Manchester United imeratibiwa kuchuana na Leicester jumapili ijayo. (Habari hii ni kwa hisani ya BBC Swahili) |
No comments:
Post a Comment