DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, September 11, 2014

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE ZA SEKONDARI DSM

Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 4.5, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Sekondari Manispaa ya Temeke, Yasintha Kayoza kwa niaba ya shule tatu za Sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (mwenye miwani), akiangalia moja ya vitabu vya masomo ya sayansi baada ya kuvikabidhi vitabu vyenye thamani ya milioni 4.5, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 1.5, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana. Sekondari nyingine zilizokabidhiwa vitabu hivyo ni pamoja na Mvuti na Kambangwa. Kushoto ni Mwakilishi wa Shule ya Sekondari Kambangwa, Mwalimu Sueiba Mfinanga.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbagala wakifurahia vitabu vya masomo ya sayansi, baada ya Kampuni ya Airtel kupitia Mradi wake wa ‘Shule Yetu’ kukabidhi vitabu hivyo vyenye thamani ya milioni 4.5 kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment