DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, September 11, 2014

NGOWI AKUTANA NA RAIS KIKWETE IKULU JANA

Mbunifu wa Mavazi wa Kimataifa Sheria Ngowi (kulia) akibadilishana mawazo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Jakaya Kikwete Ikulu jana Jijini Dar es Salaam alipomtembelea na kujadili mambo mbalimbali.

Rais Kikwete akipitia baadhi ya sampuli za vitambaa vya nguo vinavyotumiwa na mbunifu wa mavazi wa kimatafaifa Sheria Ngowi (kulia) Ikulu Jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Sheria Ngowi Brand Haki Ngowi.

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe Maalum Kutoka Sheria Ngowi Brand ukiongozwa na Mbunifu wa Mavazi wa Kimataifa, Sheria Ngowi (wa pili kushoto) Makamu wa Rais wa Sheria Ngowi Brand, Haki Ngowi (wa pili kulia) Mkuu wa Kitendo cha Biashara na Matangazo Deo Kessy (wa kwanza kushoto) na Kiongozi wa Idara ya Habari kutoka Sheria Ngowi Brand Atunza Nkrulu (wa kwanza Kulia). Picha zote na Freddy Maro -IKULU

No comments:

Post a Comment