DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, September 11, 2014

NFRA KANDA YA DODOMA INAKABILIWA NA UFINYU WA ENEO LA KUHIFADHIA MAZAO

Baadhi ya Magari ya mizigo yakipakua mahindi na mtama kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma.

Moja ya maghala ya NFRA Kanda ya Dodoma ambayo yamejaa mahindi na Mtama na hivyo kuhitaji maeneo/maghala mengine zaidi ya kuhifadhia mazao.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikagua shughuli za ufungashaji wa mahindi na mtama kwenye magunia tayari kwa kuhifadhiwa kwenye maghala wakati alipotembelea kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma jana.

Akinamama kwenye Kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma wakipeta mahindi na kuyaondoa uchafu tayari kwa ajili ya kuyafungasha kwenye magunia na kuyahifadhi ghalani, mahindi hayo yananunuliwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara mbalimbali.

Lori lililobeba mahindi likipima uzito tayari kwa mazao hayo kupeleka ghalani kwa ajili ya kuhifadhiwa kwenye maghala yaliyopo kwenye kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma, changamoto kubwa kituoni hapo ni uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akitafakari kwa kina huku akiwa ameshika gunia la mahindi hasa baada ya kujionea wingi wa mazao yaliyopo kwenye Kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma huku kituo hicho kikikabiliwa na changamoto kubwa ya uchache wa maghala ya kuhifadhia chakula.

Vijana kwenye kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma wakiendelea na shughuli za kufungasha mahindi na mtama kwenye magunia kwa ajili na kuyahifadhi ghalani, mazao hayo yananunuliwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara mbalimbali, changamoto kubwa kituoni hapo ni uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa vyama mbalimbali vya ushirika vya kilimo vilivyoleta mazao kuuza kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, mapema jana wakati ukaguzi wa zoezi la ununuzi wa mazao kituoni hapo.


Magari yaliyobeba mahindi na mtama yakiwa kwenye foleni nje ya kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakisubiri kuuza mazao hayo kwa wakala huyo wa serikali kama walivyokutwa kituoni hapo jana.

No comments:

Post a Comment