Mario Balotelli akipambana jana Anfield
KLABU ya
Liverpool imeifunga Middlesbrough kwa penalti 14-13 katika Raundi ya
Tatu ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup kufuatia sare ya 2-2
ndani ya dakika 120 Uwanja wa Anfield. Kinda
Jordan Rossiter alianza kuwafungia Wekundu hao baada ya kupewa nafasi ya
kwanza kuchezea kikosi cha kwanza, kabla ya Adam Reach kuwasawazishia
wageni akimalizia pasi ya Grant Leadbitter. Mchezo huo ulihamia kwenye muda wa nyongeza kufuatia timu kumaliza zikiwa zimefungana 1-1 baada ya dakika 90. |
No comments:
Post a Comment