PICHANI ni mapokezi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliyerejea nchini kwake (Kenya) jana baada ya kuhudhuria Mahakama ya Kimataifa ICC, iliyopo The Hague nchini Uholanzi. Kenyatta alikanusha
mashtaka dhidi yake ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu kuhusiana na ghasia
za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, zilizosababisha vifo vya watu wapatao 1,200
na wengine 600,000 kupoteza makazi. Kenyatta anakuwa rais wa
kwanza aliyepo madarakani kufika katika mahakama ya ICC. Aidha, akihutubia umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza kumpokea, Kenyatta alihimiza umoja, mshikamano, kusameheana na kuyatatua matatizo ya nchi hiyo kwa pamoja.
|
No comments:
Post a Comment