DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, September 11, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AKAGUA VIFAA NA ENEO MAALUMU KWA WAGONJWA WA EBOLA JIJINI DAR ES SALAAM


Baadhi ya wahudumu waliovalia mavazi maalumu wa  wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola iliyoko katika eneo la Hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam hivi karibuni.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaangalia wahudumu waliopata mafunzo maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa Ebola wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola iliyopo katika eneo la Hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaamhivi karibuni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wauguzi waliovalia mavazi maalumu tayari kutoa huduma kwa  abiria  atakayekutwa na ugonjwa wa Ebola  mara atapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi madaktri na wauguzi walivyo jiandaa kufanya ukaguzi wa abiria na kutambua wagonjwa wa Ebola mara watakapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam hivi karibuni.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi vifaa maalumu vinavyofanya kazi ya kutambua wagonjwa wa Ebola mara watakapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment