DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, October 08, 2014

DKT. SHEIN AMTIMUA KAZI MWANASHERIA MKUU SMZ

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein amemteua Mhe. Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, Dkt Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Mheshimiwa Said Hassan anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman ambaye Uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53, 54 (1) na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Kifungu 12(3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011. Kabla ya Uteuzi huo Mhe. Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Uteuzi huo umeanza tarehe 07, October, 2014.
 IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment