DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, November 30, 2015

DEWJI ATUNUKIWA TUZO YA MTU WA MWAKA AFRIKA NCHINI AFIRKA KUSINI

Mwanzilishi na mchapishaji wa jarida la Forbes Afrika, Bw. Rakesh Wahi ( wa pili kushoto) akikamkabidhi Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji (wa pili kulia) tuzo ya Heshima Barani Afrika "2015 Forbes Africa Person of the Year" iliyotolewa na Jarida la Forbes Afrika kwa kutambua mchango wake katika kusaidia jamii ikiwemo kutoa ajira kwa zaidi ya watu 26,000 nchini na mambo mengine yanayoigusa jamii. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Forbes Afrika, Sid Wahi (kulia) na MEC Panyaza Lesufi kutoka kitengo cha elimu, Gauteng Province (kushoto).

Mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akitembea kwenye 'Red Carpet' mara baada ya kuwasili katika hotel ya Hilton Sandton jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwenye hafla ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na jarida maarufu la Forbes na kutunukiwa tuzo ya "Forbes Africa Person Of the Year 2015".
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa nje ya ukumbi wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na jarida la Forbes. (Picha ni kwa hisani ya mrokim.blogspot.com)

VIONGIZI KUJADILI ATHARI ZA JOTO DUNIANI LEO

Mazungumzo kuhusu Mabadiliko ya tabia nchi yanaanza rasmi asubuhi ya leo huko jijini Paris nchini ufaransa, wakuu wa nchi zaidi ya mia na hamsini wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo uliondaliwa na umoja wa mataifa.
Maandamano yamefanayika duniani kote kushinikiza kuchukuliwa hatua kupambana na ongezeko la joto duniani, jijini Paris Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji huku watu mia moja wakishikiliwa kwa kosa la kukiuka amri ya kutofanya maandamano iliyotolewa baada ya mashambulizi jijini humo.
Akifungua mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, alisema ana uhakika kuwa mazungumzo hayo yatawafikisha kwenye hatua ya makubaliano chanya.
Wakati huo huo rais Obama amezuru kituo cha burudani cha Bataclan mjini Paris kutoa heshima zake kwa waathiriwa na shambulio la kigaidi wiki mbili zilizopita. Obama na rais wa nchi hiyo, Francois Hollande waliweka shada la maua kwenye ukumbi huo, ambako watu tisini waliuawa na wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki.

RAIS DKT MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA WA TRA RISHED BADE BAADA YA KUSABABISHA HASARA YA BILIONI 80 BANDARINI

Raisi wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Rished Bade kufuatia kasoro kubwa za kiutendaji zilizobainika katika Mamlaka ya Mapato nchini.Rais amechukua uamuzi huo hivi karibuni baada ya ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Majaliwa Kasimu Majaliwa katika Bandarini jijini Dar es Salaam.Kasoro hizo ni pamoja na na kuingizwa nchini kwa makontena zaidi ya 300 ambayo hayajalipiwa ushuru na hivyo kusababisha upotevu wa zaidi ya shilingi bilioni 80 za mapato ya serikali.Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue,alisema kufuatia kusimamishwa kazi kwa bade, Rais amemteua Dk. Philip Mpango kuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA).Kabla ya uteuzi huo, Dk Mpango alikuwa Katibu Mtendaji wa tume ya Mipango.Pamoja na hatua hizo Balozi sefue amsema Raios Magufuli ameagiza watu wote ambao wanajijua kuwa wameingiza nchini makontena ya bidhaa mbalimbalipasipo kulipa ushuru na kodi kama inavyopaswa waende wenyewe katika mamlaka ya Mapato Tanzania kulipa ushuru unaopaswa.Wakati huohuo Balozi Sefue amesema safari zote zawafanyakazi wa TRA nje ya nchi zimefutwa na badala yake amewataka wafanyakazi hao kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi zaidi katika mamlaka hiyo ukiendelea.

KLEYAH AZINDUA VIDEO MPYA YA 'MZOBE MZOBE' AKIMSHIRIKISHA BARNABA BOY

Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi kipya  Maarufu  kama Bongo Fleva KLEYAH ambaye anakuja kwa kasi katika Tasnia hiyo  hatimaye amezindua wimbo wake mpya unaoitwa MZOBE MZOBE. Katika wimbo huo amemshirikisha msanii maarufu kutoka THT Barnaba Boy CLASSIC wimbo ambao unatabiriwa kufanya vizuri katika soko la musiki wa Tanzania.

KLEYAH ambaye ni Mhitimu wa Shahada ya Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Phoenix nchini Marekani na baadae kufanya kazi katika shirika la kimataifa la UNDP kabla ya  kuacha na kuamua kurejea nchini kwa ajili ya kuendeleza na kukuza sanaa yake Tayari amefanikiwa kufanya kazi na watayarishaji na wasanii wakubwa ambapo mwaka 2014 alifanikiwa kufanya nyimbo mbili ambazo zilirekodiwa nchini Kenya na mtayarishaji maarufu nchini humo Lucas Bikedo pamoja na kufanyia Video kwa watayarishaji maarufu nchini Kenya kwa sasa OGOPA DJS.

Katika wimbo wake mpya ambao ulizinduliwa tarehe Novemba 6 na kuchezwa katika vituo mbalimbali vya Radio nchini Tanzania na Africa mashariki kwa ujumla na hatimaye Novemba 26, 2015 umefanyika uzinduzi wa Video yake ya wimbo wa MSOBE MSOBE unataraji kutambulishwa katika vituo mbalimbali vya Televission kwa ajili ya kumtambulisha msanii huyo ambaye anaonekana kuja kwa kasi katika sanaa hii ya music wa kizazi kipya.Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Video hiyo KLEYAH amesema kuwa kwa sasa mipango yake ni kuendelea kufanya kazi pamoja na watayarishaji wakubwa nchini Tanzania pamoja na wasanii maarufu ili kukamilisha santuli yake ambayo amepanga kuizindua mwezi Julai mwaka 2016. Santuli hiyo ambayo ametamba kuwa itasheheni aina mbalimbali za muziki ili kuwafurahisha mashabiki wanaofuatilia kazi zake.

Ameongeza aliamua kufanya muziki kwa kuwa ni kitu ambacho kipo ndani ya moyo wake huku akieleza kuwa kusoma na baadae kufanya muziki ni jambo la kuigwa na wasanii wa Tanzania kwani itamsaidia msanii kutoboa tu si ndani ya nchi lakini Barani Afrika na duniani kwa ujumla.

VIJANA IRINGA WAWEZESHWA NA AIRTEL FURSA‏

Mshiriki wa mafunzo ya Airtel Fursa mkoani Iringa Bi Fatuma Mkini (kushoto ) akipokea cheti cha ushiriki wa mafonzo hayo kutoka kwa afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki mara baada ya mafunzo ya Airtel Fursa kumalizika mkoani Iringa kwa vijana zaidi ya 200 kushiriki.
wawakilishi wa vijana zaidi ya 200 mkoani Iringa walioshiriki kupata mafunzo ya ujasiriamali kupitia mradi wa Airtel fursa wakiwa katika picha ya pamoja na afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki na wafanyakazi wengine wa Airtel mkoa wa Iringa mara baada ya kukabidhiwa vyeti kwa niaba ya wenzao.
...............Baada ya kukata tamaa ya maisha kwa muda mrefu baadhi ya vijana mkoani Iringa wameeleza kufurahishwa na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa kuwapatia mafunzo ya jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara zao kwa faida kupitia mpango wa Airtel FURSAWakizungumza na mara baada ya mafunzo ya siku moja ya Airtel FURSA yaliyofanyika katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa kwa kuwashirikisha vijana zaidi ya 200,washiriki hao walisema kuwa mafunzo hayo ni ukomb0zi mkubwa kwao kwani baadhi yao walikuwa wakilazimika kushinda vijiweni kutokana na kukosa fursa ya mafunzo kama hayo .Washiriki wa mafunzo hayo Bi Husna Sanga na Bw Okelo Kasim wakizungumza kwa niaba ya wenzao walisema kuwa mbali ya kuwa wa hatua ya kampuni hiyo ya simu ya Airtel kutoa mafunzo hayo si tu kunawasaidia kupata elimu kuendesha biashara na miradi mingine ya kiuchumi bali ni sehemu ya ukombozi kwao na familia zinazowazunguka .Alisema Bi Sanga kuwa sehemu kubwa ya vijana hasa mabinti walikuwa wakirubunika na kujiingiza katika biashara zisizofaa kama za uuzaji wa miili yao kutokana na kutokuwa na elimu ya uanzishaji wa biashara ndogo ndogo ambao zingewakomboa kiuchumi hivyo kupitia mpango huo wa Airtel FURSA ni wazi kilio chao kimepata majibu.“Wapo baadhi ya mabinti wenzetu ambao wanalazimika kufanya biashara ya kuuza miili yao ili kupata kipato na mwisho wa siku wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa UKIMWI , ila kwa sisi ambao tumepata elimu hii kupitia Airtel FURSA tunaweza kuwa mfano kwa wengine ambao wanafikiri kazi ni kuuza miili yao pekee”Huku Bw Kasim mbali ya kupongeza kampuni ya simu ya Airtel Tanzani kwa kuwakumbuka vijana bado alisema kuwa kama njia ya wao kupongeza kampuni hiyo ya simu kwa vijana wote waliopata mafunzo hayo kwenda kuonyesha mfano kwa wenzao kwa kufanya kazi ya kubuni miradi na kuendesha shughuli zao kifanisi zaidi.Kwa upande wake afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki kuwa Kutokana na mradi huo wa Airtel FURSA vijana wengi watanufaika zaidi na wanafaidika na mradi huo ni wale wenye miaka kati ya 18-24Alisema kuwa mradi huo umelenga kuwafikia vijana kote nchini na hadi sasa zaidi ya mikoa tisa wamefikiwa na mradi huo wa Airtel FURSA .Bi Kaniki alitaja mikoa ambayo tayari imefikiwa na mradi huo Mbeya, Arusha, Dodoma, Mtwara, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam , morogoro, Tanga, Tabora na Iringa kuwa hadi sasa zaidi ya vijana 1700 wamefikiwa.Alisema kuna njia mbili za kuwawezesha vijana njia ya kwanza kupatiwa Mafunzo ya ujasiriamali na njia ya pili kupatiwa vitendea Kazi .Hivyo aliwataka vijana wote nchini ambao watasikia taarifa ya kuwepo kwa Airtel Fursa katika Mkoa wao basi kuweza kuchangamkia Fursa hiyo ambao hutolewa bure.Alisema ili kijana aweze kufaidika au kushiriki kwenye Airtel FURSA atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepeairtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara.Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.comAlisema kuwa Airtel Fursa inawalenga vijana ambao wapo katika biashara na wale ambao hawana shughuli na wanataka kuanzisha shughuli pia kwao ni fursa kwao .Aidha alisema kuwa tayari baadhi ya vijana wamepata kunufaika na mradi huo ambao umelenga kuwainua vijana na kuongeza kuwa mradi huo ulioanza mwaka huu utakuwa ni mradi endelevu.

PAPA FRANCIS NCHINI KENYA

Papa Francis akiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiangalia burudani ya ngoma ya utamaduni mara tu alipowasili uwanja wa ndege wa kimatiafa wa Jomo Kinyetta nchini humo Novemba 25, 2015.
Papa Francis akizungumza jambo na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya baada ya kuwasili nchini humo ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku sita kwa nchi za Afrika za Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati,  huku Papa akitarajiwa  kueneza ujumbe wake wa Amani, maridhiano, mashauriano na kuchochea juhudi za kuzima migawanyiko. Kushoto ni Mke wa Rais Kenyatta, Margaret Kenyatta na kulia ni Naibu Rais wa Kenya, William Ruto.

Afisa wa mawasiliano wa Vatican Padri Federico Lombardi alisema kwamba kwa Jorge Mario Bergoglio, ambalo ndilo jina kamili la Papa Francis, hii itakuwa ziara yake ya kwanza kabisa Afrika.
Hii ni ziara ya 11 ya Francis akiwa papa nje ya Vatican. Mapapa wawili wamewahi kuzuru mataifa haya kabla yake.


Friday, November 27, 2015

WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA BANDARINI

Ni gumzo ndani ya kazi ya Rais mpya awamu ya tano ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye kila siku amekuwa kwenye vichwa vya habari wa magazeti kwa kukata bajeti na kupunguza matumizi ya serikali kwenye vitu kadhaa.

Sasa leo Novemba 27, 2015 Waziri Mkuu aliyemteua juma liliyopita Dodoma, Majaliwa Kassim Majaliwa ameamuru kukamatwa kwa Maafisa wote wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliohusika na wengine kufukuzwa kazi  baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta ubadhirifu mkubwa.
Maafisa hao ambao kwa sasa majina yao yamehifadhiwa ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri ambapo hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo yapo kwenye kumbukumbu za mamlaka ya Bandari lakini katika mtandao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hayaonekani.
Habari kamili inaandaliwa kutoka Ikulu.
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa 
akiagana na viongozi wa TRA na TPA. CHANZO: Millardayo.com

MRADI WA 'SAFARI SATELLITE CITY' WAPATA MAJI KWA UJENZI WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU 100

Uongozi wa Shirika Mkoa wa Arusha umefanikisha uvutaji wa bomba la maji safi kutoka umbali wa Kilomita1.5 kama sehemu ya kuwezesha mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika mji mdogo wa Safari City kuanza mwaka ni kama ilivyopangwa.
Hatua hiyo muhimu imechukuliwa kutokana na ukosefu wa maji katika eneo hilo la Safari City na gharama kubwa ya kupeleka maji kutoka eneo la mashamba ya Magereza ambapo Shirika linalenga kusukuma zaidi ya lita 3,000,000 kwa siku ili kutosheleza mahitaji ya jiji lote huko baadaye.
Aidha, kiasi cha lita 100,000 ambayo imewekewa hifadhi inatosheleza kabisa kwa malengo ya sasa ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa lengo la kuutangaza mji huo na kuwapeleka wakazi wengi kwa muda mfupi.
Wafanyakazi  wa Shirika ofisi ya Mkoa wa Arusha wakifurahia mafanikio hayo ya maji kufika katika mradi wa Safari City. Kufika kwa maji haya kunaashiria kuanza kwa mradi wa ujenzi wa  nyumba za gharama nafuu ambazo zilikwama kutokana na ukosefu wa maji.
Wafanyakazi wakipata maelezo na ufafanuzi zaidi kuhusu matumizi ya maji hayo, ukubwa wa hifadhi hiyo ya maji na uwezo wa kuhudumia zaidi ya nyumba 100 bila tatizo lo lote.  Hifadhi hiyo ni ya lita 100,000 na upo uwezo wa kuongeza maji kila siku kwa karibu lita 60,000.
Maji ya kuendeleza mradi wa Safari City yakizinduliwa rasmi na Meneja wa Mkoa wa Arusha, Ndugu James Kisarika tarehe 24/11/2015. Jirani wa kwanza kupata maji hayo ni mama  Sophia Rajab.
Picha inamwonyesha inamwonyesha mama Sophia Rajabakisaidiwa kubeba maji yake na Ndugu Kisarika.   
Baadhi ya wakina mama wakiwa katika foleni na  ndoo zao wakisubiri kupata maji kwa mara ya kwanza kabla ya uzinduzi. Katika muda usiozidi dakika moja presha ya maji hujaza ndoo ya lita 20.

JK AWASILI OFISINI KWAKE LUMUMBA

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ofisini kwake Makao Makuu ya  CCM Ofisi Ndogo Lumumba.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.

JPM ATINGA OFISINI KWA MAJALIWA

Rais Dkt. John P. Magufuli aweka saini  kitabu cha wageni wakati alipomtembelea Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015  na kuzungumza nao kwa takribani saa moja (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Rais Dkt. John P. Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Rais Dkt. John P. Magufuli akiagana  na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Friday, November 20, 2015

MKALI WA MOVIE KUTOKA HOLLYWOOD JEAN CLAUDE VAN DAMME AWATEMBELEA MAN CITY WAKIWA MAZOEZINI

Staa wa movie kutoka Hollywood Jean-Claude Van Damme mkali ambaye amewahi kutamba na movie kadhaa  jana Novemba 19 alipata nafasi ya kutembelea mazoezi ya Klabu ya Manchester City. Staa huyo wa Hollywood yupo jijini Manchester kwa ajili ya shughuli ya ‘black-tie dinner’ ambapo atapata nafasi ya kuoneshwa kwa movie zake.
Jean-Claude Van Damme ambaye ana umri wa miaka 55 alivyotembelea mazoezi ya Man City mastaa wa klabu hiyo hawakuacha kuchukua kumbukumbu zao kwa kupiga picha na staa huyo, wachezaji wa Man City kama Yaya ToureVincent KompanyKevin De BruyneSergio Aguero pamoja na kocha wao Manuel Pellegrini hawakusita kupiga picha na Van Damme.
Jean-Claude Van Damme na Vincent KompanyMkali huyo wa movie duniani ambaye kwa miaka ya karibuni ametamba katika tangazo la bia, amewahi kutamba katika movie za mapigano zikiwemo BloodsportHard Targetna Universal Soldier. Hizi ni baadhi ya pichaz zake alivyotembelea Man City.
Sergio Aguero na Jean-Claude Van Damme.
Jean-Claude Van Damme Kevin De Bruyne.
Jean-Claude Van Damme na golikipa wa Man City Joe Hart.
Kocha wa Man City Manuel Pellegrini akiwa na Jean-Claude Van Damme.
Jean-Claude Van Damme katika miaka ya 1990 alitamba sana na movie iliyokwenda kwa jina la Universal Soldier. Movie hiyo aliicheza  pamoja na Dolph Lundgren.

UN WAZINDUA MRADI WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI, CHAMWINO DODOMA


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akipanda mti kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimwagilia maji kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo (kulia) wakieleka kukagua mradi wa ufugaji wa shirika la Tanzania Environmental Friendly Association (TEFA) huku wakiburudishwa na ngoma ya wenyeji wa kabila wa Kigogo, katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma, Zena Mwalko baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa kwenye picha ya pamoja na wanakikundi cha ngoma cha Kijiji cha Machali A, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo.

DKT. TULIA AKSON MWASASU AWA NAIBU SPIKA WA BUNGE 11


Na Lilian Lundo, Maelezo DodomaWabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemchagua Mhe. Dkt. Tulia Akson kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Naibu Spika wa Bunge la 11 baada ya kumshinda mpinzani wake kutoka Chama cha Wananchi (CUF) Mhe. Magdalena Sakaya.Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mhe. Dkt. Akson kushinda kwa kura 250 ambazo ni sawa na asilimia 71.2 za kula halali dhidi ya mpinzani wake Mhe. Sakaya aliyepata kura 101 ambazo ni sawa na asilimia 28.8 ya kura halali.Uchaguzi huo umefanyika leo, Mjini Dodoma ambao ulitanguliwa na uthibitisho wa jina la Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.Akiomba kura kwa wabunge Mhe. Dkt. Akson alisema kuwa atajitahidi kuwatunukia wananchi wote bila kujali tofauti za kisiasa ili kuwaletea wananchi maendeleo.Aliongeza kuwa atajitadi kumshauri vizuri Spika juu ya Sheria na Kanuni kwa kutumia uzoefu alionao kama Mwanasheria mzoefu ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wote.Akimpongeza Mhe. Dkt. Akson Tulia kwa ushindi alioupata, Mhe. Sakaya alisema kuwa matarajio yake na watanzania ni kuona nchi inakuwa na Bunge imara litakalo fanya kazi zake kwa uimara bila ubaguzi ili kuiletea nchi maendeleo.Akitoa neno la shukurani mara baadaya kuchaguliwa Mhe. Dkt. Akson alimshukuru Mhe. Rais kwa uteuzi alioufanya wa kumteua kuwa Mbunge na hatimaye kugombea nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la 11.“Naahidi nitawatumikia kama mtumishi wenu, tutafanya kazi kiufanisi na pia nitatumia weledi wangu katika kazi zangu kama Naibu Spika, naomba msisite kuniletea hoja zenu pale mnapokuwa nazo,” alisema Mhe. Dkt . Akson.Kabla ya kuchaguliwa kuwa Naibu Spika Mhe. Dkt. Akson alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Thursday, November 19, 2015

MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU

Mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa ndiye Waziri Mkuu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania. 
Majaliwa ambaye ni Mwalimu kitaaluma na Serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete alikuwa Naibu Waziri -Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (ELIMU).  
 Majaliwa amefanya kazi kama Naibu waziri na Agrey Mwanry chini ya Tamisemi, wakiwa chini ya mawaziri George huruma Mkuchika-2010-2012, Hawa Ghasia-2012-2015.
Majaliwa pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo.Majaliwa amekuwa Mbunge wa Ruangwa tangu 2010 na alizaliwa Desemba 22, 1960. 
Alisomea ualimu chuo cha Ualimu Mtwara na mafunzo ya JKT alifanyia kambi ya Makutopora mkoani Dodoma. 
Alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aliwahi kuwa Katibu wa Chama cha walimu Singida. Bunge litarejea baade kwaajili ya kulipigia kura jina hilo. 


TANESCO: ZOEZI LA KUDHIBITI WIZI WA UMEME KUANZA NCHI NZIMA

Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani)mapema leo jijini Dar es Salaam kuhusu mpango wa Serikali wa kuunda kikosi maalum cha kukabiliana na tatizo la wizi wa umeme na kuimarisha ukaguzi ili kubaini wateja wasio waaminifu na kuwachukulia hatua za kisheria. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa. (Picha na Fatma Salum- Maelezo).***************Na Greyson Mwase, Dar es SalaamKutokana na wizi wa umeme kukithiri na kuliingizia hasara Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wizara ya Nishati na Madini imeliagiza Shirika hilo kuimarisha kikosi chake cha ukaguzi wa watumiaji wa umeme ili kubaini wateja wasio waaminifu wanaoiba umeme na kuwachukulia hatua za kisheria.
 Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya  Nishati na Madini Badra Masoud alipofanya mkutano na waandishi wa habari  kwa  ajili ya kuendelezea  mafaniko na changamoto katika usimamizi  wa sekta ya  umeme.Masoud alisema Wizara inatarajia kuunda kikosi maalum kitakachojumuisha wataalam kutoka katika taasisi mbalimbali kwa ajili  ya  kukabiliana na tatizo hilo linalolikosesha mapato shirika la TANESCO.
Alisema  kikosi hicho kitajumuisha wataalam kutoka TANESCO, Wizara ya Nishati pamoja na vyombo vya usalama na kuongeza kuwa hatua hii imekuja baada ya Wizara kubaini kuwa kuna  baadhi ya watu wanaohujumu miundombinu ya TANESCO kama vile kuchoma nguzo za umeme, kuiba mafuta ya transfoma pamoja na nyaya za umeme  na kuwataka  kuacha kufanya hujuma hizo kwani watakaogundulika wataendelea kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akielezea  zoezi  hilo, Masoud alisema kuwa  hivi sasa sasa vyombo vya dola katika mkoa wa Lindi vinaendelea kuwasaka na kuwatia nguvuni wale wote waliohusika kuchoma nguzo za umeme wa msongo mkubwa unaosafirisha umeme kutoka Mtwara kwenda Lindi katika vijiji vya Hingawali na Njonjo mkoani Lindi na kusababisha mikoa hiyo miwili kukosa umeme na kusababisha hasara kwa TANESCO.Masoud alizitaka  Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Kiserikali kuzingatia matumizi bora ya umeme ili kudhibiti upotevu wa nishati ya umeme na kusisitiza kuwa  utaratibu huu wa matumizi bora ya umeme hufanywa pia na nchi nyingi duniani kwa ajili ya kukabiliana na upotevu wa umeme.
Aliongeza kuwa kuna baadhi ya taasisi huwa zinaacha umeme ukiendelea kupotea baada ya muda wa kazi kama vile kuacha  viyoyozi, taa, kompyuta na vifaa vingine vinavyotumia umeme vikiendela kutumia umeme hivyo  kusababisha  upotevu mkubwa  wa umeme ambao  ungetumika katika maeneo mengine au kuokoa fedha ambazo hutumika kuzalisha umeme huo.
Akielezea hali ya upatikanaji wa umeme nchini  Masoud alisema kuwa  hali ya umeme nchini ni nzuri na hakuna mgawo wowote unaoendelea hivi sasa kwani hali ya uzalishaji ni nzuri pamoja na mabwawa ya maji ambayo hutumika kuzalisha umeme kukauka.
Alisisitiza kuwa kiasi cha umeme kinachopatikana kwa sasa ni megawati 1500 huku matumizi ikiwa ni kati ya megawati 800 na 900 kutokana na umeme huo kuzalishwa kwa kiasi kikubwa kutokana na gesi asilia pamoja na mafuta mazito na dizeli.

SBC YAPUNGUZA BEI YA VINYWAJI VYAKE

NA BEATRICE LYIMO-MAELEZO,
 Dar es Salaam.

Kampuni ya SBC Tanzania Limited, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji baridi imepunguza bei ya vinywaji vyake kutoka shillingi mia sita (600) hadi mia tano (500) kwa chupa yenye ujazo wa Mililita 350 na 300.Hayo yamesemwa na Meneja Mafunzo na Uwezeshaji Bw.Rashid Chenja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa lengo la kupunguza bei ni kutokana na hali ngumu ya uchumi iliyopo.“Imekuwa vigumu kwa mnywaji kuweza kudumu bei ya kinywaji akipendacho cha pepsi , gharama za maisha zinapanda kila mwaka na soda imekuwa ghali kiasi cha wananchi wa kawaida kushindwa kumudu kununua soda hivyo kampuni imeamua kupunguza bei” alifafanua Meneja huyo.Pia amesema kuwa kampuni ya SBC Tanzania imefanya punguzo hilo  kuanzia tarehe 16/11/2015 kwa vinywaji vya Pepsi, Mirinda,7up, Mountain Dew na Evervess na maeneo yatakayo husika na punguzo hilo la bei ni Dar es salaam,Morogoro, Dodoma, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara na Zanzibar.“Ni matumaini yetu mtaendelea kutuunga mkono katika biashara yetu kwa kununua soda zetu kwa bei iliyopendekezwa ya shilingi Mia Tano kwa chupa, shilingi elfu tisa mia nne (9,400) kwa kreti moja na faida kwa wauzaji wa rejareja itakuwa ni shilingi 2500 kwa kila kreti” aliongeza Bw. Chenja. 
Mbali na hayo Kampuni ya SBC Tanzania Limited inawashukuru wateja wake kwa kuwaunga mkono katika biashara yao kwa kipindi cha miaka 14 hapa nchini.