Ni gumzo ndani ya kazi ya
Rais mpya awamu ya tano ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli ambaye kila siku amekuwa kwenye vichwa vya habari wa magazeti kwa kukata
bajeti na kupunguza matumizi ya serikali kwenye vitu kadhaa.
Sasa leo Novemba 27, 2015 Waziri Mkuu aliyemteua juma liliyopita Dodoma, Majaliwa Kassim Majaliwa ameamuru kukamatwa kwa Maafisa wote
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliohusika na wengine kufukuzwa kazi baada
ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta ubadhirifu mkubwa.
Maafisa
hao ambao kwa sasa majina yao yamehifadhiwa ili Jeshi la Polisi liweze
kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri ambapo hii
imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya
zaidi ya bilioni 80 ambayo yapo kwenye kumbukumbu za mamlaka ya Bandari
lakini katika mtandao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hayaonekani.
Habari kamili inaandaliwa kutoka Ikulu. |
No comments:
Post a Comment