Papa Francis akizungumza jambo na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya baada ya kuwasili nchini humo ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku sita kwa nchi za Afrika za Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku Papa akitarajiwa kueneza ujumbe wake wa Amani, maridhiano, mashauriano na kuchochea juhudi za kuzima migawanyiko. Kushoto ni Mke wa Rais Kenyatta, Margaret Kenyatta na kulia ni Naibu Rais wa Kenya, William Ruto.
Afisa wa mawasiliano wa Vatican Padri Federico Lombardi alisema kwamba kwa Jorge Mario Bergoglio, ambalo ndilo jina kamili la Papa Francis, hii itakuwa ziara yake ya kwanza kabisa Afrika.
Hii ni ziara ya 11 ya Francis akiwa papa nje ya Vatican. Mapapa wawili wamewahi kuzuru mataifa haya kabla yake.
|
No comments:
Post a Comment