Wakati Taifa Stars wanatafakari namna ambavyo watasawazisha magoli Mudathir Yahaya alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 41, kipindi cha pili kocha wa TanzaniaBoniface Mkwasa alifanya mabadiliko ya kumuingiza Aishi Manula na kumtoa golikipaAly Mustapha na Farid Mussa nafasi yake ikachuliwa na Salum Telela, mabadiliko ambayo hayakuzaa matunda.
Magoli ya Algeria yalifungwa na Yacine Brahimi dakika ya 1, Faouzi Ghoulam dakika ya 23 na dakika ya 59 akapachika goli jingine kwa mkwaju wa penati, Riyad Mahrezdakika ya 43 na Islam Slimani kafunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 49 na 75, Carl Medjani dakika ya 72 . Kwa matokeo hayo Taifa Stars imetolewa kwa jumla ya magoli 9-2 baada ya mchezo wa awali kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
|
No comments:
Post a Comment