Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein
|
Mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa visiwani Zanzibar yameendelea huku mkutano uliowaleta pamoja Rais Ali Mohammed Shein na kiongozi wa upinzani Seif Sharif Hamad ukifanyika.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, mkutano huo wa faragha katika Ikulu ya Rais ulihudhuriwa na marais wa zamani Ali Hassan Mwinyi na Amani Abeid karume.
Ni mara ya kwanza kwa Dkt. Shein ambaye anatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Bw. Seif wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye ni Makamu wa Rais wa kisiwa hicho kukutana tangu tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo ya urais.
Kushirikishwa kwa marais hao wa zamani ni uthibitisho kwamba kuna harakati za kisiasa zinazoendelea katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo ambalo limezua mgogoro wa kikatiba.
Wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa pia wanadaiwa kushiriki katika kumaliza tatizo hilo.
Hakuna habari zilizotolewa kutoka pande zote mbili lakini duru za serikali zimethibitisha kwamba mazungumzo hayo yalifanyika kwa faragha.
No comments:
Post a Comment