DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, November 10, 2015

KENYA: BODABODA MARUFUKU JIJINI NAIROBI

Bodaboda marufuku katikati ya Jiji la Nairobi Kenya! Katikati ya Jiji la Dar es Salaam zoezi hili lilianza muda mrefu zaidi ya mwaka mmoja umepita, ambapo ilipigwa marufuku kabisa madereva wa bodaboda na Bajaji kuonekana wakisafirisha wateja wao kuingia katikati ya Jiji hilo. 
Habari hiyo imeripotiwa na Kituo cha Televisheni cha K24 ambapo madereva wa bodaboda wenyewe wameonekana kulalamikia agizo hilo wakisema kwamba wanazuiliwa kuingia katikati ya Jiji la Nairobi lakini hawajaoneshwa wapi ni eneo rasmi haswa ambapo wanatakiwa kufanya  shughuli zao.
Kingine ambacho kimetangazwa Nairobi ni kwamba mkikamatwa mnakatisha katikati ya Nairobi, abiria pamoja na dereva wote mnapigwa faini

No comments:

Post a Comment