DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, November 11, 2015

NEC: VYOMBO HABARI VIMECHANGIA KUFANYA UCHAGUZI MKUU KUWA WAZI, HAKI NA HURU

Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Giveness Aswile, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuvishukuru vyombo vya habari kwa kuripoti vizuri katika kipindi chote cha uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani. 
Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Giveness Aswile, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuvishukuru vyombo vya habari kwa kuripoti vizuri katika kipindi chote cha uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Emmanuel Kavishe.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)imesema kuwa waandishi wamechangia kufanya uchaguzi kuwa haki na uhuru kutokana na kutoa taarifa zao bila kuegemea upande. 
 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya sheria wa NEC, Emmanuel Kawishe amesema kuwa mwenendo wa uchaguzi tume ilifanya kuwa wazi kwa kuhakikisha wananchi wanapata habari kupitia vyombo habari.
 Amesema kuwa NEC haina uwezo wa kufikia watu milioni 26 kutokana na kuwepo kwa vyombo vya habari kwani vimekuwa ni daraja la kufanya wananchi wafikiwe na habari kwa wakati.
 Kawishe aliongeza kuwa katika kipindi chote cha uchaguzi amekuwa akishiri katika vyombo habari katika kutoa taarifa kwani bila kufanya hivyo zoezi la upigaji kura lisingekuwa rahisi kama wananchi wasingepata elimu ya mpiga kura.
 ’’Upigaji wa kura umeisha napita kwa kujidai na watu wengi wananikaribisha katika kushiriki hata kunywa kahawa nisingefanya hivyo kama vyombo vya habari vingeongea vibaya kuhusu mimi juu ya elimu niliyokuwa nikitoa katika vyombo hivyo.’’amesema Kawishe.
 Nae Mkuu wa Idara ya Habari NEC, Giveness Aswile amesema katika uchaguzi ujao watajipanga waandishi waweze kufika sehemu zote ili wananchi wajue kazi za tume.
 Amesema Tume imekuwa wazi na kufanya waandishi wajitume katika kutoa taarifa ambazo zimefanya uchaguzi kuwa wa wazi na huru zaidi kwa kupata habari katika kila hatua ambayo tume ilikuwa ikifanya.

No comments:

Post a Comment