Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi kipya Maarufu kama Bongo Fleva KLEYAH ambaye anakuja kwa kasi katika Tasnia hiyo hatimaye amezindua wimbo wake mpya unaoitwa MZOBE MZOBE. Katika wimbo huo amemshirikisha msanii maarufu kutoka THT Barnaba Boy CLASSIC wimbo ambao unatabiriwa kufanya vizuri katika soko la musiki wa Tanzania.
KLEYAH ambaye ni Mhitimu wa Shahada ya Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Phoenix nchini Marekani na baadae kufanya kazi katika shirika la kimataifa la UNDP kabla ya kuacha na kuamua kurejea nchini kwa ajili ya kuendeleza na kukuza sanaa yake Tayari amefanikiwa kufanya kazi na watayarishaji na wasanii wakubwa ambapo mwaka 2014 alifanikiwa kufanya nyimbo mbili ambazo zilirekodiwa nchini Kenya na mtayarishaji maarufu nchini humo Lucas Bikedo pamoja na kufanyia Video kwa watayarishaji maarufu nchini Kenya kwa sasa OGOPA DJS.
Katika wimbo wake mpya ambao ulizinduliwa tarehe Novemba 6 na kuchezwa katika vituo mbalimbali vya Radio nchini Tanzania na Africa mashariki kwa ujumla na hatimaye Novemba 26, 2015 umefanyika uzinduzi wa Video yake ya wimbo wa MSOBE MSOBE unataraji kutambulishwa katika vituo mbalimbali vya Televission kwa ajili ya kumtambulisha msanii huyo ambaye anaonekana kuja kwa kasi katika sanaa hii ya music wa kizazi kipya.Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Video hiyo KLEYAH amesema kuwa kwa sasa mipango yake ni kuendelea kufanya kazi pamoja na watayarishaji wakubwa nchini Tanzania pamoja na wasanii maarufu ili kukamilisha santuli yake ambayo amepanga kuizindua mwezi Julai mwaka 2016. Santuli hiyo ambayo ametamba kuwa itasheheni aina mbalimbali za muziki ili kuwafurahisha mashabiki wanaofuatilia kazi zake.
Ameongeza aliamua kufanya muziki kwa kuwa ni kitu ambacho kipo ndani ya moyo wake huku akieleza kuwa kusoma na baadae kufanya muziki ni jambo la kuigwa na wasanii wa Tanzania kwani itamsaidia msanii kutoboa tu si ndani ya nchi lakini Barani Afrika na duniani kwa ujumla.
|
No comments:
Post a Comment