DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, November 10, 2015

CRISTIANO RONALDO AZINDUA FILAMU IITWAYO 'RONALDO'

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayesakata kabumbu katika klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania, Cristiano Ronaldo usiku wa Novemba 9 alifanya uzinduzi rasmi wa filamu yake ambayo ametaja kuiandaa kwa ajili ya mashabiki wake. Ronaldo amefanya uzinduzi wa filamu yake hiyo inayoitwa ‘Ronaldo’ akiwa pamoja na mama yake na mtoto wake Cristiano Ronaldo Junior.
Ronaldo akiwa na mtoto wake Cristiano Ronaldo Junior mwenye umri wa miaka mitano.Uzinduzi huo uliyofanywa Leicester Square jijini London Uingereza na ulihudhuriwa na makocha wa zamani wa staa huyo ambao ni Sir Alex FergusonJose Mourinho na Carlo Ancelotti sambamba na uwepo wa wakala wake Jorges Mendes na mastaa wengine wengi.
Ronaldo akiwa na kocha wake wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson aliyekuwepo katika uzinduzi huo.Filamu hiyo ambayo imechezwa kwa zaidi ya miezi 14 kwa asilimia kubwa inahusisha maisha halisi ya staa huyo ambaye alianzia maisha yake ya soka katika Klabu ya Sporting Lisbon ya UrenoRonaldo amefanya uzinduzi huo sambamba na kufanya mahojiano mafupi katika zulia jekundu (red carpet).
Cristiano Ronaldo akiwa na mama yake Maria Dolores Aveiro na mtoto wake katika zulia jekundu.
Ronaldo, Carlo Ancelotti na Jorges Mendes.
Jose Mourinho.
Radamel Falcao na mkewe.
Ronaldo akikabidhiwa tuzo ya kuwa mtu anayeongoza kwa kupata 'like' nyingi zaidi duniani katika mtandao wa facebook.
Gary Neville.
Ronaldo na mtoto wake.

No comments:

Post a Comment