Uongozi wa Shirika Mkoa wa Arusha umefanikisha uvutaji wa bomba la maji safi kutoka umbali wa Kilomita1.5 kama sehemu
ya kuwezesha mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika mji mdogo wa
Safari City kuanza mwaka ni kama ilivyopangwa.
Hatua hiyo muhimu imechukuliwa kutokana na ukosefu wa maji
katika eneo hilo la Safari City na gharama kubwa ya kupeleka maji kutoka eneo
la mashamba ya Magereza ambapo Shirika linalenga kusukuma zaidi ya lita
3,000,000 kwa siku ili kutosheleza mahitaji ya jiji lote huko baadaye.
Aidha, kiasi cha lita 100,000 ambayo imewekewa hifadhi inatosheleza
kabisa kwa malengo ya sasa ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa lengo la
kuutangaza mji huo na kuwapeleka wakazi wengi kwa muda mfupi.
|
No comments:
Post a Comment