DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Saturday, March 29, 2014

MBIO ZA UBUNGE CHALINZE: RIDHIWANI AFUNIKA KATA YA PERA


Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akipunga mkono juu huku Mzee Kazidi ambaye ni Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro na Meneja wa Kampeni wa mgombea huyo akicheza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo kwenye kata ya Pera.

Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi katika viwanja vya kwa Mwarabu kata ya Pera Chalinze leo wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, Unaotarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu jimboni humo, Ridhiwani amewaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo ifikapo Aprili 6 ili aweze kuwatumikia na kuleta maendeleo ya jimbo hilo akishirikiana na wananchi kwa ujumla wake uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Said Ramadhan Bwanamdogo. (Picha na MjengwaBlog)

RC DODOMA DR. REHEMA NCHIMBI AKAGUA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA NHC KONGWA

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Alfred Msovella akimuongoza Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi wakati akikagua ujenzi wa ndani  wa nyumba za shirika la nyumba la Taifa unaotekelezwa Wilayani Kongwa. Jumla ya nyumba 44 zenye mchanganyiko wa vyumba viwili na nyingine vitatu zinatarajiwa kukamilika Aprili 2014 na kuuzwa kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (katikati waliosimama mbele) akiwa na viongozi wa Wilaya ya Kongwa na wataalamu wa ujenzi wa NHC wakifanya majumuisho mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba 44 za shirika la nyumba wilayani Kongwa.


Baadhi ya nyumba za shirika la nyumba la Taifa zinazojengwa eneo la Mnyakongo kwenye mji wa Kongwa, mradi huo una jumla ya nyumba 44 ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 80, zitakamilika mwezi April 2014 na kuuzwa kwa wananchi.

Friday, March 28, 2014

MATUKIO YA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KITAIFA YALIVYOFANA DODOMA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa serikali na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Dodoma muda mfupi mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa mkoani humo hivi karibuni.

Wanafunzi wametambua umuhimu wa maji na rasilimali zake hivyo waliitikia wito na kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa mkoani Dodoma hivi karibuni.

Baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa baadhi ya  vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Dodoma wakipata ufafanuzi juu ya pampu za kuvuta na kusukuma maji. Elimu juu ya vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya maji, uhifadhi na utunzaji vyanzo na rasilimali za maji zilitolewa kwa wingi kwenye maadhimisho hayo yaliyoambatana na maonesho ya huduma za maji kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Teknolojia rahisi ya uvunaji maji ya mvua kwenye majengo/makazi yetu ni moja kati ya elimu iliyowavutia wananchi wengi wakati wote wa maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa mkoani Dodoma yaliyoambatana na maonesho ya huduma za maji kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma hivi karibuni.

Mkuu wa mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi ( nyuma mwenye miwani) akiwa pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi mkoani dDodoma wakishangilia kuhitimishwa kwa maadhimisho ya wiki ya Maji kitaifa mkoani Dodoma hivi karibuni, wanafunzi walionesha kuelewa umuhimu wa vyanzo na rasilimali za maji kwa jamii.