Rais wa Bayern Munich amehukumiwa kwenda jela kwa
kifungo cha miaka mitatu na miezi sita kutokana na kosa la kukwepa kodi.
Uli Hoeness, 62, alikiri kukwepa kodi inayofikia
kiasi cha €18.5 million kupitia akaunti zake za benki za siri lakini utetezi
wake wa kukiri kosa akidhania ungemsaidia kuepukana na adhabu ya kifungo
ulishindwa kumsaidia.
Mwndesha mashtaka alitaka Hoeness afungwe jela miaka mitano na nusu kwa
kutokana na kupatikana na hatia ya kukwepa kodi.
Mwishowe, Jaji wa mahakama iliyokuwa ikisikiliza
kesi hiyo akaamuru mwanasoka huyo wa zamani wa Ujerumani Magharibi atumikie
kifungo cha miaka 3 na miezi sita
|
No comments:
Post a Comment