TAARIFA KWA UMMA
Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Marehemu Mhe. John
Gabriel Tuppa unatarajiwa kuwasili Mjini Dodoma kwa njia ya ndege leo Alhamisi
tarehe 27 Machi 2014 majira ya saa kumi na nusu jioni ukitokea mkoani Mara kwa
kupitia Mwanza. Baada ya mwili kuwasili uwanja wa ndege wa Dodoma, utapokelewa
na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi ambapo utapelekwa kwenye chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Ratiba ya siku ya Ijumaa ya tarehe 28 Machi 2014 ni kwamba,
mwili wa marehemu utapelekwa kwenye uwanja wa Nyerere Square kuanzia saa tatu asubuhi ambapo pataendeshwa Ibada ya kuuaga
mwili wa marehemu na kutoa salamu za rambirambi na baadaye kuuaga mwili wa
marehemu. Shughuli nzima ya tarehe 28 Machi 2014 itaanza saa tatu kamili
asubuhi na kukamilika saa nane kamili mchana ambapo safari ya kuelekea Kilosa, Morogoro
ambako Mazishi yatafanyika tarehe 29 Machi 2014.
Hivyo, wananchi wanaombwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi
uwanjani wakati wa kuupokea mwili wa marehemu na siku ya kuuaga mwili wa
marehemu pale Nyerere Square.
“Mwanga wa Milele
Umwangazie Ee Bwana Apumzike kwa Amani Ndugu yetu Mhe. John Gabriel Tuppa,
Amina”
TAARIFA HII IMETOLEWA
NA KAMATI YA URATIBU YA MSIBA YA MKOA WA DODOMA
27 Machi 2014
No comments:
Post a Comment