Leo ni ' Super Sunday!'
Kuna ndoto zitakufa leo. Katika vyombo vya habari vya Uingereza, leo ni 'Super
sunday!' Ni kwa kuwa kuna mechi mbili kali sana!
Ni Manchester United dhidi ya Liverpool, na Arsenal dhidi ya Tottenham. Kwa
mtazamo wangu, mechi ya kwanza niliyoitaja hapo juu ni muhimu zaidi. Ukweli ni
huu: kama Manchester United wanafungwa au wanatoka sare leo, basi, nafasi yao
ya kuchukua nafasi ya nne ni ndogo sana, na wakifungwa naamini watashindwa
kuchukua nafasi hii.
Vile vile mechi hii ni muhimu sana kwa Liverpool. Kama Liverpool wanashinda
leo naamini watacheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Na kama Liverpool
wanashinda, Brendan Rodgers atabadilisha lengo lake. Mwanzoni mwa msimu huu
Brendan Rodgers alisema lengo la Liverpool msimu huu ni kuchukua nafasi ya nne.
Lakini, kama Liverpool wanawafunga Manchester United ugenini, bila shaka
'The reds' wana nafasi na uwezo wa kushinda ligi na hii itakuwa lengo la
Rodgers. Arsenal pia wana ndoto ya kushinda ligi msimu huu.
Jana Chelsea walifungwa na Aston Villa na kwa hiyo, Arsenal wanaweza
kupunguza pointi ambazo wanazihitaji kuwafikisha Chelsea. Lakini, kama Arsenal
wanafungwa leo, 'The gunners' watakuwa na mlima mkubwa kuwakamata Chelsea, Man
City na labda hata Liverpool.
Vile vile kama Manchester United, Tottenham pia wana ndoto na lengo la
kuchukua nafasi ya nne. Kwa sasa wameshika nafasi ya tano lakini Arsenal ambao
wapo katika nafasi ya nne wamewapita kwa pointi sita na Tottenham wamewazidi
Arsenal mechi moja. Kwa hiyo, ni muhimu sana kwamba Tottenham hawafungwi.
Waingereza wana msemo: 'The ball is round'. Wana maana, kwamba chochote
kinaweza kutokea katika mpira. Na chochote kinaweza kutokea katika mechi za
leo. Siwezi kutabiri matokeo ya mchana huu, lakini, ninachojua ni kwamba,
lazima kuna ndoto zitakufa leo!
Na Olle Bergdahl Mjengwa,
Stockholm
|
No comments:
Post a Comment