Kaimu Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania
anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne
(CSEE) na Maarifa (QT) mwezi Novemba, 2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea
kwamba kipindi cha usajili kwa malipo ya ada ya kawaida (Shilingi 50,000/=kwa wanaojisajili
CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT ) kimeongezwa kutoka tarehe 28
Februari, 2014 hadi tarehe 31 Machi, 2014.
Watahiniwa watakaojisajili kuanzia tarehe 1 Aprili, 2014
hadi tarehe 30 Aprili, 2014 watatakiwa kulipa ada
ya kawaida pamoja na faini mpaka usajili utakapofungwa rasmi
tarehe 30 Aprili, 2014.
Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema
kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz Kabla ya kujisajili kwenye
mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba
rejea (reference number) zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya
Posta au Mpesa.
Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA.
No comments:
Post a Comment