Sheria nchini Uganda inawakataza wanawake kuvaa nguo fupi za kuonyesha
sehemu zao za siri
Wanawake wawili jana walizuiliwa
kwa saa 3 na mahakama moja nchini Uganda kwa kuingia mahakamani wakiwa
wamevaa 'Mini Skirt'. Hii ni baada ya jaji aliyekuwa
mahakamani humo kusema kuwa wanawake hao walikuwa wamevaa nguo zisizofaa.
Kwa mujibu wa taarifa kwenye mtandao
wa Daily Nation, nchini Kenya, Bi Prosy Nasuna aliyekuwa amemshitaki Bi. Jane
Nabukenya kwa kukosa kumlipa deni lake la shilingi milioni 3 za Uganda wote
ilisemekana hawakuvaa nguo za heshima na kutatiza kikao cha mahakama.
Walipoingia mahakamani katika eneo
la Bukomansimbi jana Prosy pamoja na mshitakiwa walijikuta matatani.
Kabla ya kuchukuliwa hatua kwa
mavazi yao, watu walipiga mayowe mahakamani humo wakisema kuwa wawili hao
walikuwa wamevaa visivyo kulingana na sheria iliyopitishwa mwezi Februari, 2014
kuhusiana na kupiga marufuku mavazi mafupi. Sheria hiyo inasema kuwa yeyote
atakeyeonesha sehemu za siri za mwili wake hadharani na kusababisha hisia
fulani miongoni mwa watu, anakuwa amekiuka sheria.
Minong'ono na kelele za watu
zilisababisha hakimu kuamuru kukamatwa kwao kwa kwenda kinyume na sheria na pia
kwa kuhujumu wa mahakama. Alisema kuwa kesi haikuendelea
kutokana na mavazi yao na kwa hivyo kosa lao lilikuwa kusababisha usumbufu
mahakamani kwa kuvaa 'Mini Skirt'.
Hakimu aliwahukumu jela kwa saa 3 wanawake hao na
kuahirisha kesi yao hadi Machi 13,2014. (Chanzo ni BBC Swahili).
|
No comments:
Post a Comment