Shughuli ya kuitafuta ndege ya Malaysia ikiwa inaendelea
Maafisa
nchini Malysia wanaendelea kuitafuta ndege iliyotoweka
wakati ikitokea Kuala Lumpur kuelekea Beijing siku Jumamosi iliyopita.
Siku tatu baada ya ndege hiyo kutoweka, chini ya saa moja kabla ya
kufika
mwisho wa safari yake, juhudi za kimataifa zinazohusisha meli na ndege
za
kutafuta mabaki ya ndege hiyo bado hazijafanikiwa.
Makundi ya uokozi kutoka mataifa tisa kwa sasa yataangaza maeneo ya Malacca
na Bahari ya Kusini ya Uchina. Maafisa wa Serikali ya Malaysia wamesema kuwa watu wawili waliosafiri kwa
ndege hiyo wakitumia paspoti iliyoibwa wametambuliwa.
Siku ya Jumatatu, ndege moja ya Vietnam imeripoti kuwa imeona kitu
kinachofanana na mlango wa ndege kwenye ufuo wa bahari ya Kusini mwa Uchina
kwenye mwambao wa taifa hilo. Hata hivyo hakuna uthibitisho kuwa mlango huo ni wa ndege iliyopotea ya
Malaysia, iliyokuwa na abiria 239.
Uchunguzi kuhusiana na kilichosababisha kupotea kwa ndege hiyo mapema siku
ya Jumamosi, unawalenga abiria wawili wanaodaiwa kuwemo ndani ya ndege hiyo,
waliotumia paspoti iliyoibiwa.
Stakabadhi hizo mbili za kusafiria kutoka Italia na nyingine Australia
inaaminika ziliibwa nchini Thailand lakini Idara ya Polisi ya Kimataifa, Interpol, inasema kuwa ni mapema mno kuhusisha
pasi zilizoibwa na kutoweka kwa ndege hiyo.
Wakuu
wa Malaysia wanasema jumla ya meli 30 na ndege 44 kutoka mataifa tisa
tofauti duniani, yamejiunga katika shughuli za kuitafuta ndege hiyo.
Kamanda William Marks wa Kikosi cha Saba cha Jeshi la Wanamaji la
Marekani,
ametuma ndege aina ya USS Pinckney kusaidia katika usakaji huo. Japo ameonya kuwa shughuli hiyo ya kutafuta ndege
hiyo inakumbwa na changamoto nyingi. (Habari na picha kwa hisani ya BBC Swahili)
No comments:
Post a Comment