DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Sunday, March 16, 2014

RC DODOMA ATEMBELEWA NA UJUMBE KUTOKA BUNGE LA KOREA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akimshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Korea Bw. AHN Hong  Joon (kushoto) mara baada ya kupokea zawadi yenye heshima kwa asili ya watu wa korea kutoka kwa kiongozi huyo ambaye aliambatana na ujumbe kutoka Bunge la Korea na Shirika la Kimataifa la Misaada la Korea-KOICA. Ujumbe huo ulimtembelea mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma ofisini kwake hivi karibuni kuzungumzia masuala ya ushirikiano na maendeleo.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akielezea fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Dodoma kwa ujumbe kutoka Bunge la Korea wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya bunge hilo Bw. AHN Hong Joon (wa pili kulia). Ujumbe huo wa Bunge la Korea hivi karibuni ulimtembelea Mkuu wa Mkoa Dodoma kuzungumzia masuala ya Ushirikiano na maendeleo.

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) na ujumbe kutoka Bunge la Korea wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Korea Mr. AHN Hong Joon (wa pili kulia waliokaa). Ujumbe huo ulimtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma hivi karibuni kuzungumzia masuala ya ushirikiano na maendeleo.

No comments:

Post a Comment