DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, March 11, 2014

MGIMWA ANAENDELEA NA KAMPENI TOSAMAGANGA NA KALENGA LEO

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu akihutubia wakazi wa Kitongoji cha Tosamaganga wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa Ubunge Jimbo la Kalenga kupitia tiketi ya CCM Ndugu Godfrey Mgimwa ambapo aliwaambia wananchi hao kuchagua viongozi wa mfano kwa Kitanzania.
Diwani wa Kata ya Kalenga Ndugu Maria Galinoma akihutubia wakazi wa Kitongoji cha Tosamaganga wakati wa kumnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Ndugu Godfrey Mgimwa.
Msanii maarufu Tanzania mwenye vipaji vya kuigiza, kucheza na kuimba Dokii akiimba na kucheza pamoja na Diwani wa Viti Maalum ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Iringa Vijijini, Ndugu Shakira Kiwanga wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge za CCM kwenye Kitongoji cha Tosamaganga.
Chifu Abdul Adam Sapi Mkwawa akiwahutubia wakazi wa Kalenga A, wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge kupitia CCM na kusema yeye mpaka kufa kwake ni CCM na kamwe asitafsiriwe vinginevyo.

No comments:

Post a Comment