Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha ujumbe wa Mawaziri na Wakuu wa
Taasisi za Uhifadhi nchini kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Kimataifa wa
Kuzuia Biashara Haramu ya Wanyamapori jijini London, Uingereza. Mkutano wa Kimataifa kuhusu Biashara Haramu ya Wanyamapori (Conference on
Illegal Wildlife Trade) unaanza rasmi leo katika ukumbi wa Lancaster House. Mkutano huo utahudhuriwa na mataifa 47 na Mashirika 13 ya Kimataifa na umeitishwa na Serikali ya Uingereza kwa lengo la kujadili masuala maalum matatu kuhusiana na biashara haramu ya wanyamapori.
|
No comments:
Post a Comment